Friday, June 29, 2012

UNAMWAMINI VIPI MPENZI WAKO NA PASSWORD ?

Katika siku za karibuni tumekuwa na kesi nyingi za wapenzi kuibiana fedha , nyaraka na siri nyingine kwa njia ya mtandaohaswa simu ,barua pepe na mifumo mengine mbalimbali ya mawasiliano .

Kitu kilichogunduliwa baada ya uchunguzi mwingi ni kwamba wapenzi

wengi wanaaminiana sana haswa wanawake kuamini sana wapenzi wao wa kiume kiasi kwamba atampa password za email yake , kadi yake ya benki na hata siri za kazini kwake kisa anaogopa kuachwa .

Tukumbuke kwamba password au neno la siri ni mali ya mtu binafsi na ni
yako wewe mwenyewe , ukienda benki ukapewa password au neno la siri kwa ajili ya kadi yako ya benki ni wewe umeingia mkataba na benki sio mpenzi wako , mdogo wako au mumeo au jirani yako .

Sikatazi watu kupeana namba za siri manake kupeana muda mwingine
unajenga kuaminiana zaidi , kupendana zaidi na hata kuweza kusaidiana katika mikasa ya hapa na pale endapo mtu ana hizo namba za siri huu ndio uzuri wa kupeana namba za siri .

Ubaya wake ni mwingi na unaweza kuwa mchungu zaidi katika maisha yako
yote , kwa mfano mtu akakuta picha zako au nyaraka nyingine za siri kwenye email zako akaamua kuzihifadhi sehemu nyingine kwa kuzichukuwa baadaye ukaona picha hizo kwenye magazeti , blogu na sehemu nyingine za kijamii , kwa nyaraka au namba za siri za benki mtu anawezakuchukuwa na yeye mwenyewe akaenda kukuibia hela au anaweza kumtumiamtu mwingine ndani ya benki au nje kwa ajili ya kuhamisha fedha haswakiasi kikubwa cha fedha na usimwone tena pengine haswa kama mmeokotana njiani .

Kama wewe ni muajiriwa na ukampa mpenzi wako password ya anuani pepe
yako akafanikiwa kuangalia mawasiliano yako na wafanyakazi ,
wasimamizi wako au hata siri nyingine za unapofanyia kazi hizi
zinaweza kuibiwa na kutumika dhidi yako au dhidi ya kampuni yako au serikali yako muda wowote .

Hizo zote ni tisa kumi ni pale mpenzi wako anapoingia ndani ya barua
pepe yako na kuweka taarifa nyingine bila ya wewe kujua ili awezekuzitumia pindi mtakapoachana au kukorofichana , kwenye barua pepe yako kuna sehemu inaitwa PASSWORD RECOVERY hata kwenye simu kuna baadhi zenye huduma za Recovery .

Ukiwa kwenye barua pepe kuna kitu kinaitwa recovery Options hii

inayoweza kutumika ni kwa kuweka anuani nyingine ya barua pepe kwa ajili ya kurejesha pwd kama imepotea au imesahaulika , saa nyingine unaweza kutumia namba za simu kwa ajili ya kuweza kurudisha password yako .

Unapomwachia mpenzi wako password yako anaweza kuingia kwenye barua
pepe yako na kubadilisha hizo taarifa pale kwenye recovery email ataweka yake unayoijua au usiyoijua , kwenye namba za simu anaweza pia kuweka zake . ikiwa ndio hivi ataweza kubadilisha password muda wowote akitaka na wewe usiweze tena kuingia katika anuani hizo .

Nakumbusha tena kwa kuuliza unamwamini mpenzi wako na password ? kama
unamwamini hongera zako lakini ujue password ni mali binafsi na anuani pepe ni mali binafsi pia labda kama kuna makubaliano mengine ya ziada .

NB : Hii haihusiani na pale unapotegeshewa programu ya kunukuu na

kuhifadhi password kwenye ma internetcafe au maofisini zinazoitwa
KEYGEN . Keygen ni mada tofauti ingawa ukishtuka password yako
imeibiwa unauwezo wa kubadili password haraka .

USHAURI WANGU

Hakikisha unabadili password zako za barua pepe , kadi za benki , simu na vifaa vingine mara kwa mara na hakikisha taarifa hizo zinatunzwa na kama unashare na mtu hakikisha unakuwa na njia mbadala za kuweza kurecover namba za siri kama zimepotea mara moja la sivyo siku utakujalia .

YONA FARES MARO

0786 806028

Popular Posts

Labels