Saturday, April 13, 2019

MAMBO 10 AMBAYO YAWEZA FANYWA NA SIMU JANJA

 Related image



1.Kutune Gitaa /Kutafuta Ufunguo wa Sauti ya Gitaa
Kulikuwa na wakati ambapo bei ya  vifaa vya umeme kwa ajili ya kutafuta ufunguo wa sauti za gitaa na vifaa vingine ilikuwa ghali ,kwa sasa unachotakiwa ni kupakua program tumishi sahihi kwa ajili ya simu yako ili kukupatia funguo za sauti mbalimbali za gitaa,muafaka wa sauti na maelezo ya kutumia.

2.Ufuatiliaji wa  Mtoto akiwa amelala

Program tumishi hizi zenye akili  zitakuwezesha kuiweka simu yako ndani ya chumba cha mtoto ambapo program hiyo itamfatilia  mtoto aliyelala  kwa  kumsikiliza kama anajongea ama kutoa sauti yake,Kama mtoto atajongea ama kutoa sauti program hii tumishi itagundua kisha itapiga namba kwa mwenyenayo na atafahamu kuwa mtoto ameamka kutoka usingizini.

3. Kipima Kasi

Programu tumishi  kadhaa za Mfumo wa Dunia wa Utambuzi wa Mahali ulipo GPS zinaweza kupima kasi yako kwa usahihi sana unapoendesha lako. Mara nyingi hupangwa kuwa na ufahamu wa kikomo cha kasi katika maeneo mengi na inaweza kukujulisha ikiwa unazidi kikomo hicho. Hii inaweza kuwa na manufaa sana ikiwa kasi ya gari katika gari yako imevunjika au isiyo sahihi mfano.

4. Kipasha joto Mikono

Amini au la, kuna programu tumishi ambazo unaweza kutumia ili kuipasha joto  mikono yako wakati wa baridi,Program hizi huiongoza processor ya simu yako ili simu ipate joto,Kumbuka tu ni kwamba program tumishi hizi zinatumia uwezo mkubwa wa betri ya simu yako,hivyo ni budi uweke tahadhali

6. Kufahamu matumizi ya pombe

Ingawa inaweza kuwa sio wazo bora kuweka imani yako yote katika programu kama hii, bado inaweza kuwa na manufaa kukusaidia kupata kufahamu kiwango cha pombe alichotumia mwendeshaji wa chombo cha moto  na kusaidia kuepusha ajali

7. Vizuizi vya mwendokasi

Aina hizi za programu zinategemea idadi ya watumiaji wanaohusika ili waweze kuwa na matumizi yoyote. Watumiaji wanaweza kutoa taarifa za maeneo yenye vizuizi  ya kasi ambavyo wanaviona katika eneo fulani, na kisha kutoa taarifa kwa watumiaji wengine watumiaji wengine katika eneo hilo. Kwa kutumia GPS, itaeleza  moja kwa moja mtumiaji akikaribia eneo ambapo kuna vizuizi vya mwendo kasi uliowekwa

8.Remote

Yawezekana u miongoni mwa wanaopoteza remote ya vifaa vya kielektroniki ikiwemo Televisheni,radio,dvd,jokovu nk .Baadhi ya program tumishi zinaiwezesha simu yako na kuifanya kuwa remote ambapo itakuwaidia katika vifaa hiyo.

9.Gari Janja

Kwa sasa kuna program tumishi  ambazo zinakuwezesha kutumia simu yako kuiongoza gari kwa baadhi ya mambo ikiwemo kuwasha gari ukiwa nje ,kuwasha na kuzima alamu,kufungua na kufungua milango.

10.Utambuzi wa Vyuma

Hii ni Program Tumishi ambayo inafanya kazi katika simu janja aina ya iPhones na iPads, kuwezesha kutambua vyuma ambavyo haviwezi kuonekana kwa macho kwa urahisi katika eneo husika


Friday, April 5, 2019

UCHUNGUZI WAONESHA TATIZO LA KIMFUMO LILISABABISHA AJALI YA BOEING 737 MAX 8

 Image may contain: aeroplane

Ripoti ya awali ya uchunguzi wa ajali ya ndege la Shirika la Ndege la Ethiopia safari namba 302 inaonyesha kwamba ajali hiyo ilitokana na tatizo la kimfumo katika ndege na kwamba marubani wa ndege hiyo walifanya kila walichoelekezwa na kufuata taratibu zote kwa mujibu wa watengenezaji wa ndege hiyo lakini hawakufanikiwa kuizuia isianguke.

Mfumo katika aina ya ndege iliyoanguka (Boeing 737 Max 8 ) umekuwa katika mjadala mkubwa kiasi cha kusababisha nchi nyimgi kuamrisha kusimamishwa kwa matumizi ya ndege hizo na Wizara ya Sheria, Mkaguzi Mkuu masuala ya Usafirishaji na Kamati za Bunge la Marekani vimeanzisha uchunguzi tofauti na maalum wa namna ambavyo kampuni hiyo ilivyofanya maboresho ya mfumo na walivyopata kibali cha uthibitisho wa ubora toka Mamlaka ya Anga ya Marekani.


Ndege hiyo iliyoanguka Machi 10, 2019 na kuua abiria wote 157, ilikuwa ni ya pili ya aina hiyo kuanguka ndani ya miezi 5 na hilo likazua hofu kwa wasafiri na wasafirishaji kuhusu usalama wa ndege hizo.


Ripoti kamili inatarajiwa kutoka baadae sana, lakini punde nitakapopata nakala ya awali ya ripoti hiyo nitaileta hapa ili kushiriki nanyi juu ya dondoo za uchunguzi huo.


Shirika la Boeing linalotengeneza ndege hizo lilitangaza kwamba lingefanya maboresho ya mfumo huo hivi karibuni lakini inaonekana wamesubiri matokeo haya ili kuhakikisha wanawathibitishia wateja wake kuwa wanaboresha kile kinachowatia hofu kutokana na ajali mbili za ndege zake.

Na: Mubelwa Bandio-Marekani

Thursday, March 28, 2019

APPLE YATOA SASISHO LA PROGRAM ENDESHI YA iOS 12.2


Apple wametoa Sasisho la Program Endeshi ya  iOS 12.2  kwa ajili ya  iPhone, iPad, and iPod toleo ambalo litawezesha wenye vifaa vya hivyo kunufaika za Apple zilizotambulishwa jumatatu ya Machi 25 mwaka huu nchini Marekani ikiwemo huduma ya kupata habari iitwayo Apple News+

 Apple pia wameongeza imoji,ambapo iOS 12.2 itamwezesha mtumiaji wa huduma ya  Siri  iliyopo katika vifaa hivyo kuongoza  Apple TV kwa kutumia  iPhone au  iPad. 

 Miongoni mwa madiliko yaliyokuja na sasisho la iOS 12.2 ni kukusianisha kwa Apple News+ na Apple  News iliyokuwepo mwanzo,
 ambapo huduma hii ya kulipia itawawezesha watumiaji wa vifaa vya Apple waliopakua sasisho hili jipya kupata zaidi ya magazeti mtandao 300,na machapisho mengine ya habari ya kidigitali.

Monday, April 30, 2018

WAKUU WA TEKNOHAMA WAKUTANA KENYA



 
 


Watunga sera na sheria mbali mbali wamekua wakifanya maamuzi ya TEKNOHAMA bila kushirikisha wadau wa TEKNOHAMA – Hii imekua moja ya changamoto inayo leta mkinzano wa utendaji wenye manufaa kwa wana TEKNOHAMA maeneo mengi barani Afrika.

Mjadala ulioangazia umuhimu wa udhibiti na uangalizi wa watendaji katika sekta ya TEKNOHAMA umeonekana kua mzuri ila umegubikwa na changamoto kadhaa kutokana na ushirikishwaji mdogo wa wadau ili kuweza kuleta mabadiliko kwenye sekta husika.

Mjadala huu umejadiliwa kufuatia kuwepo kwa sera mpya nchini Kenya itakayo rasimisha Wana TEKNOHAMA na kuwataka watambulike kabla ya kuweza kuhudumu maeneo mbali mbali. Hili litafanana na tulicho nacho nchini Tanzania kwa wanasheria pamoja na wataalam wa maeneo mengine kadhaa.

Kinachotegemewa katika urasimishaji wa sekta ya TEKNOHAMA na kumfanya mwana TEKNOHAMA atambulike na kuhudumia katika sekta ya TEKNOHAMA ni pamoja na  kupitia hatua kuu tatu ambazo ni, Kusomea – Usaili – Kupatiwa leseni ya kutoa huduma katika sekta husika.

Changamoto iliyo onekana ni pamoja na uwezekano wa kuua vipaji vya wabunifu wa TEKNOHAMA ambao wamekua wakija na ubunifu wenye manufaa pasi na kua na ujuzi rasmi katika sekta husika.
Tumeshudia kuwepo kwa vijana walio somea fani nyingine tofauti na TEKNOHAMA ila baadae kuja na Mifumo mizuri ya Kitehama iliyoweza kutatua changamoto mbali mbali katika maeneo yetu tofauti na wengine waliosomea fani husika na kushindwa kuwa wabunifu wa kuleta mabadiliko katika jamii zetu.

Kuna baadhi ya Mifumo tuko nayo maeneo mengi ambayo wabunifu wake hawakua na elimu ramsi katika sekta ya TEKNOHAMA. Aidha, Swali kuu matumizi ya TEKNOHAMA ya mekua kuna ulazima mhusika kua na elimu rasmi? Ilhali kila sekta inategemea TEKNOHAMA na kuna uwezekano kila mwenye ujuzi wa fani yoyote akawa na uwezo wa kufanya vizuri kwenye mifumo ya TEKNOHAMA.

GDPR (General Data Protection Regulations) Nchi za umoja wa ulaya wana mategemeo ya kuanza rasmi matumizi ya GDPR mwishoni mwa mwezi wa tano mwaka huu wa 2018 – Lengo kuu ni kulinda faragha za raia wake.

Hatua hii inaweza kuathiri maeneo mengi duniani Afrika ikiwemo kwani tumeendelea kufanya biashara na kuhudumia mataifa ya umoja wa ulaya ambapo inahusisha taarifa za wana jumuia ya ulaya kupatikana kwetu.



Mjadala mzito wa nini tutegemee pale umoja wa Ulaya watakapo anza rasmi matumizi ya GDPR katika taasisi zetu hususan za kifedha. Namna bora ya kuweza kulinda (faragha) za watumiaji mifumo ya kitehama katika taasisi zetu ili kuondokana na tunachoweza kukabiliana nacho baada ya kuanza rasmi matumizi ya GDPR barani ulaya.

CSIRT (Computer Security Incidence Response Team) – Tumekua na changamoto ya uwepo wa vitengo mahususi vya kukabiliana na matukio ya kihalifu mtandao katika taasisi na kampuni mbali mbali. Hili linatokana na uelewa mdogo juu ya umuhimu wa vitengo hivi mahsusi vyenye jukumu la kukabiliana na uhalifu mtandao.



Umuhimu wa CSIRT, namna ya kuanzisha na majukumu yake katika kila kampuni na taasisi ni mjadala nilio uongoza kuhakiki kila mmoja anafahamu hili.

Matukio ya kihalifu mtandao katika mataifa yetu yanayopelekea upotevu wa Fedha, upotevu wa taarifa, udukuzi wa mifumo na kadhalika yamekua yakijitokeza mara kwa mara yanayo acha athari kubwa kwa taasisi za serikali na binafsi maeneo mengi duniani.

Ni wajibu wa kila taasisi na kampuni kujua ina jukumu la kujilinda dhidi ya uhalifu mtandao na namna pekee ya kufikia hapo ni pamoja na kua na kitengo wahususi chenye jukumu la ulinzi mtandao pekee ambapo kitengo husika kitaweza kuhakiki usalama mtandao unakuwepo.
Aidha, kumekua na mijadala mingine mingi sana ambayo yote ilikua na lengo la kuhakiki tuna tambua namna sahihi ya kukabiliana na changamoto nyingi zinazotokana na uwepo matumizi makubwa ya mifumo ya TEKNOHAMA yanayo rahisisha utendaji kazi katika taasisi na kampuni

Friday, September 15, 2017

APPLE YAZINDUA SIMU MPYA YA iPHONE X INAYOFUNGUKA KWA KUTUMIA USO


 Simu hiyo inaweza kujichaji bila kutumia waya na haingii maji wala vumbi.

Kampuni ya Apple imezindua simu mpya aina ya iPhone X ambayo hutumia utambulisho wa uso wako badala ya kidole kufunguka.

Apple imesema kuwa simu hiyo inayojulikana kama Iphone 10 pia inaweza kutumia utambulisho huo wa uso nyakati za usiku kufunguka na kwamba ni vigumu kuidanganya ikilinganishwa na mfumo wa kutumia kidole.

Ndio simu ghali zaidi kuzinduliwa na Apple.

Ikiwa na ukubwa wa kuhifadhi Gigabait 64 simu hiyo itagharimu £999 nchini Uingereza wakati itakapoanza kuuzwa rasmi mnamo mwezi Novemba tarehe 3.

Simu yenye ukubwa wa kuhifadhi Gigabait 256 itauzwa kwa £256 nchini Uingereza.

La kushangaza ni kwamba kampuni ya Samsung inauza simu yake ya aina ya Note 8 kwa £869 nchini Uingereza ikiwa na uwezo wa kuhifadhi Gigabait 64.

Kabla ya uzinduzi huo, Simu ya Apple iliokuwa ghali zaidi ni ile ya iPhone 7 Plus ambayo inagharimu $969 nchini Uingereza.

Mtaalam mmoja alisema kuwa uwezo wa Apple kuwashawishi wateja wake kugharamikia zaidi simu zake aina ya smartphone ni kitu cha heshima.

Simu hiyo inaweza kujichaji bila kutumia waya na haingii maji wala vumbi.

Wednesday, August 9, 2017

MFUMO MPYA WA ULIPAJI KODI YA PANGO LA ARDHI NCHINI.


 
      Wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakitoa elimu jinsi ya kutumia mfumo wa Government electronic Payment Gateway kwa watendaji wa Halmashauri ya Kinondoni.
 
Elimu ya jinsi ya kutumia mfumo mpya wa kielektroniki ikitolewa kwa watendaji wa manipaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Watendaji wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Kinondoni wakipewa mafunzo jinsi mfumo mpya wa ukusanyaji maduhuli ya Serikali utakavyokuwa unatumika.
 Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza rasmi kutumia mfumo wa kielektroniki wa Government electronic Payment Gateway (GePG) katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi pamoja na tozo nyingine zinazotokana na sekta ya ardhi nchini.
Mfumo huu utamrahisishia mwananchi kulipa kodi ya pango la ardhi popote alipo, ikiwa ni pamoja na kulipia tozo nyingine mbalimbali za sekta ya ardhi. Pia mfumo wa GePG, utamuwezesha mwananchi au mmiliki wa kipande cha ardhi, kujua anadaiwa kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi na kulipia popote alipo bila kusumbuka kufuata huduma hizo katika vituo vya makusanyo.
Majaribio ya ukusanyaji kodi ya pango la ardhi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki yalifanywa katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, baada ya mafanikio makubwa kuonekana elimu ikatolewa kwa watendaji wote wa sekta ya ardhi katika Halmashauri zote za mkoa wa Dar es salaam kabla ya zoezi hilo kuhamishiwa mikoani.
Mwananchi yeyote anayemiliki kiwanja au shamba lililopimwa na kuwa na hati, ataweza kutumia simu yake ya mkononi kujua kiasi cha kodi ya pango la ardhi anachodaiwa na kukulipa kwa kutumia simu yake ya mkononi pia.
Kwa zile huduma nyingine za sekta ya ardhi ambazo zinahusisha malipo kama vile upekuzi katika daftari la msajili (official serach), mwananchi atapaswa kutembelea ofisi za Wizara ya ardhi zilizo katika eneo lake na kupatiwa makadirio ya kulipia huduma husika pamoja na namba ya malipo itakayomuwezesha kulipia aidha kwa njia ya benki au simu ya mkononi.
Kwa sasa kikosi kazi kinachotoa mafunzo juu ya matumizi ya mfumo huu kimeshaanza kuelemisha mikoa mingine baada ya kupata mafanikio mazuri katika mkoa wa Dar es Salaam. Lengo kubwa la kutumia mfumo huu ni kuongeza ufanisi katilka ukusanyaji wa maduhuli ya serikali pamoja na kurahisisha ulipaji kodi ya pango la ardhi nchini,

Popular Posts

Labels

Habari