Saturday, December 14, 2013
MICROSOFT KUWASAIDIA WANAFUNZI WA VYUO KUPITIA STUDENT ADVANTAGE
Kampuni ya Microsft Corporation imeanzisha programu mpya ambayo itawawezesha wanafunzi kufanya mazoezi yote wanayopewa shuleni kupitia teknolojia ya habari na mawasiliano.
Kampuni hiyo imebuni programu mpya ya Student Advantage ambayo itawawezesha wanafunzi kupeana kazi za shule,mazoezi ya nyumbani na masuala yote muhimu ya kitaaluma.
Mpango huo uliotangazwa hivi karibuni wakati kampuni hiyo ikitambulisha programu ya Microsoft Office 365 Education ambayo inakadiriwa kutumiwa na zaidi ya wanafunzi milioni 110 wa vyuo 35,000,idara na wahadhiri mbalimbali duniani.
Programu hiyo itawapa fursa wanafunzi kuitumia kupitia huduma zilizopo ambazo ni Microsoft Word na OneNote ambazo zinafanana na huduma za PowerPoint na Excel.
Mpango huo umeanza rasmi Desemba Mosi mwaka huu,huku vyuo mbalimbali duniani vikipewa leseni ya Office 365 ProPlus kwa wanafunzi wahadhiri pamoja na wakuu wa idara watakuwa wanatumia programu yenye leseni ya Office Proffesional Plus bila gharama zozote.Huduma hizo zote zitawapa wanafunzi nafasi wanafunzi kupata maarifa mbalimbali kupitia mtandao wakiwa nyumbani na huduma nyingine ambazo zipo kwenye programu hiyo yenye vitu vingine vitakavyomwezesha mwanafunzi kuwasiliana na wanafunzi wengine waliopo katika vyuo mbalimbali duniani.
Mkuu wa Kampuni hiyo katika nchi za Afrika Mashariki na Kati Mark Chaban anasema wamefanikiwa kutembelea vyuo 30 binafsi na vya umma pamoja na Wizara mbalimbali za elimu ili kutoa mafunzo kuhusu utumiaji wa programu hiyo ambayo ipo chini ya International Data Corporation (IDC) ambayo itakuwa ikikusanya taarifa za maendeleo ya wanafunzi watakaokuwa wakitumia ili waweze kupata ajira na kuboresha maisha yao.
Kampuni hiyo imesema inakusudia kufuatilia uwezo wa wanafunzi katika kutumia huduma hiyo ambapo watakaoonekana kuwa na kiwango cha juu watachukuliwa na kupelekwa kwenye makampuni mbalimbali na kulipwa mishahara minono.
Microsoft imepanga kutengeneza ajira kwa asilimia 28 ifikapo mwaka 2020 ambapo miongoni mwa wanafunzi milioni 115 watakaoajiriwa kwa vigezo vilivyowekwa .