iPhone 5S iliyotoka mwaka huu imetengenezwa mfumo wa kiusalama wa utambuzi wa alama za vidole,inahitaji kidole cha mmiliki kufungua simu,mfumo huu unasaidia kuzuia mwizi kuifungua simu ili kuitumia,simu hiyo pamoja na vifaa vingine vya mawasiliano vya Apple vinapopotea waweza kufahamu vilipo kwa kufuata hatua zifuatazo
Hatua # 1 – Seti na uactivate “Find My iPhone” katika kifaa chako
Hatua hii inahitajika uifanye mara unaponunua kifaa chako iwe ni Iphone,Ipad n.k.Hakikisha umepada ID yako ya Apple ambayo inahusiana na kitambulisho cha kifaa ulichokinunua,ID ambayo pia itakusaidia wakati wa matumizi katika iCloud na upakuaji wa program tumishi toka Apple.
Nenda Settings ==> iCloud ==> angalia kama “Find My App” iko ON
Utakapoweka ON “Find My iPhone” kama kifaa chako kitaibwa ama kupotea kitakusaidia kukutafuta na kufahamu kilipo .
Hatua #2 – Jiunge na iCloud.com kwa kutumia Apple ID yako
Unaweza kukitafuta na kukipata kifaa chako kilipo kwa kutumia iCloud.com iwapo utakuwa umefanya setting ya kwanza ya hatua ya kwanza kwa kufungua tovuti hiyo kwenye komputa yako na kuingia kwa kutumia Apple ID ile uliyosajili kifaa chako.Inakubali katika komputa za Window na MacHatua #3 –Fungua “Find My iPhone” na chagua palipoandikwa Device to Track
Bofya kwenye alama ya “Find My iPhone” katika ukurasa wa iCloud.comHatua # 4 – Tafuta eneo kilipo kifaa chako. Kama ni eneo la karibu na ulipokipoteza ama ni ofisini,nyumbani n.k bofya palipoandikwa "play sound to find"
Chagua picha ya miongoni mwa kifaa kilichopotea Iphone,iPad n.k mahali palipoandikwa “My Devices”. Baada ya kuchagua hapo, itaonekana ramani ya mahali kifaa kilipo ama muda wa mwisho kifaa hicho kilipokuwa.Hatua # 5 – Ruhusu “Lost Mode”. Subiri mlio wa simu na endelea kuifuatilia ilipo
Baada ya kuchagua “Find My iPhone” program tumishi kwenye iCloud itakuonesha mwongozo mwingine wa hatua zifuatazo,# Play Sound – Hapa kifaa kitaanza kitatoa mlio na kama umepoteza nyumbani,ofisini n.k utausikia mlio
# Lost Mode –Kama unauhakika kuwa umeisahau simu yako ya iphone mahali utakaoruhusu hatua hii itumike itakuomba uweke namba ya simu ambapo watu watakupata,ama unaweza kuweka sentensi ama kuacha vivyo hivyo na kubofya "Done" na ujumbe utatokea kwenye simu yako iliyopotea hata kama umeifunga na utasomeka "Hii Iphone imepotea tafadhari nipigie "Namba yako"
# Erase iPhone – Hatua ya mwisho.Kwa kutumia iCloud na Find My iPhone unaweza kufuta ama kuondoa taarifa zako katika kifaa chako kilichoibwa ambapo utaondoa email zako,program tumishi ulizoweka n.k Kumbuka hatua hizi zote zinahitaji upatikanaji wa intaneti