Utafiti unaonesha kuwa Vijana kati ya miaka 16-18 nchini Uingereza
wanaonekana kutovutiwa na mtandao wa kijamii wa facebook kutokana na kukerwa na mtandao huo.
Tovuti ya yahoo imesema kuwa Vijana hao sasa wameonekana kuvutiwa Zaidi na mitadao ya kijamii mingine ambayo ni Twitter, Instagram, Snapchat na WhatsApp.
Profesa Daniel Miller kutoka Chuo Kikuu cha London ambaye
alisaidia kufanya utafiti kuhusu jambo hilo amesema wakati ambapo wazazi
wamekuwa na wasiwasi kuhusu watoto wao kujiunga na face book lakini watoto
wanaeleza kuwa ni familia zao ndizo zinazosisitiza wawepo kwenye mtandao huo
kwa ajili ya mawasiliano.
Utafiti huo ulifadhiliwa na umoja wa ulaya na kuwahusisha
vijana wenye umri wa miaka 16-18 umeonesha kuwa mitandao mingine ya kijamii na
program tumishi zinaonekana si bora katika miongozo ya namna ya kuitumika kuliko facebook.
Utafiti huo unaonesha kuwa Facebook inawaunganisha watumiaji
vyema,inatoa mpangilio mzuri wa picha na mpangilio wa mahusiano miongoni mwa
watumiaji.
WhatsApp inaonekana
ni bora kwa ujumbe wa maandishi ambapo kwa sasa inaonekana kuipiku facebook na
kutokana na kuonekana bora katika huduma ya ujumbe mfupi wa maneno .
Miongoni mwa vijana wengi nchini Uingereza sasa wanatumia Snapchat,ambao hukuwezesha kutuma picha ambazo
huondoshwa sekunde chache baada ya kuzituma.
Kumekuwa na lawama kuhusu faragha katika mtandao wa facebook
hasa baada ya mwaka huu kuelezwa kuwa Wakala wa Ulinzi wa Marekani (NSA)
imekuwa ikifanya udukuzi wa taarifa
zilizoko katika mtandao huo.
Utafiti huo pia unaonesha kuwa vijana hao sasa wanajiunga na
Instagram mtandao unaotoa huduma ya kubadilisha picha,Mike Butcher kutoka
Techcrunch.com ameiambia Sky News kuwa Facebook ilikuwa mahali tulivu na
faradha hasa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na wahitimu kwa ajili ya kutengeneza
kipato na imekuwa maarufu.
Anaeleza kinachotokea sasa ni vijana kutafuta mitandao
mbadala ambayo ni Instagram na Twitter.