skip to main |
skip to sidebar
KAMA HAUKUJUA BASI JUA
Na MBUKE TIMES
Neno HACKER makusudio yake haswa sio kumaanisha mtu anayefanya vitendo
vya kihalifu kwa kutumia kompyuta, yaani kama vile kuiba password za
watu, kusoma emails za watu n.k. Bali neno HACKER kiasili lina maana ya
mtu mwenye uwezo wa kipekee wa kutafuta suluhu ya tatizo kwa haraka, kwa
mbinu za ubunifu ambazo pengine si mbinu rasmi, ila zinaleta suluhu ya
haraka.
--Hata hivyo kwakuwa HACKER ana ujuzi wa hali ya juu wa
matumizi ya kompyuta na ni mtundu, basi wapo Hackers walioamua kutumia
ujuzi huo kufanya uhalifu, na ndipo jina lilipoharibika.
--Hata
hivyo jamii ya hackers na wanateknolojia wengi wameendelea kuelimisha
matumizi sahihi ya jina HACKER na neno HACKING. Mifano ya wazi ni :-
1. Facebook: Kuta za ofisi za FB zimeandikwa neno HACK. Kusisitiza
umuhimu wa kuandika codes kwa haraka na kutafuta kwa ubunifu na kwa
haraka suluhu ya matatizo.
Hata mfumo mzima wa uendeshaji wa FB umepewa jina THE HACKER WAY.
2. Makampuni mengi yamekuwa yakiandaa mikutano ya siku moja au zaidi
kwa ajili ya kukutanisha HACKERS ili kubuni bidhaa na kutatua matatizo
mbalimbali. Mikutano hiyo huitwa HACKATHONS
-- Kwa maelezo zaidi search Google maneno HACKER, FACEBOOK THE HACK WAY na HACKATHONS.