Serikali ya Kenya imesema watu
watakaopatikana na hatia ya kutuma ujumbe wa kingono kwa kutumia simu za
kiganjani na intaneti watafungwa Jela.
Adhabu hiyo itawahusu wale wanaotuma
ujumbe wenye picha za watu walio uchi na zenye mada ya ngono nchini humo.
Maafisa wakuu wa serikali wanasema
kuwa yeyote atakayepatikana na hatia atafungwa jela kifungo cha miezi mitatu
kwenda chini.
Afisa mkuu kutoka tume ya mawasiliano
ya Kenya , Christopher Wambua, ameviambia vyombo vya habari nchini humo ,kwamba
watu wenye tabia hiyo ya kutuma ujumbe wa kingono ,pamoja na picha zenye watu
walio uchi ,watatozwa hadi shilingi elfu hamsini za Kenya au dola miatano na
themanini na nane za kimarekani sawa na shilingi laki tisa arobaini elfu na mia nane za
kitanzania kama faini au kufungwa jela.
Onyo hilo litawahusu hasa wale walio
na uzoefu wa kutumiana ujumbe kama huo kupitia kwa simu ya kiganjani au kwenye intaneti.
Kwa mujibu wa taarifa za serikali,
kiwango ambacho watu hutumiana ujumbe wenye mada ya ngono pamoja na picha za
watu walio uchi, zao wenyewe au za mtu mwingine kwa simu zao za kisasa ilipanda
hadi asilimia sitini.
Chanzo:BBC