Friday, May 30, 2014

POLISI WA VISIWA VYA SOLOMONI WAUNGANISHA NGUVU KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA UHALIFU MTANDAO

Polisi wa visiwa vya kifalme vya Solomon vilivyopo pasifiki ya kusini wameunganisha nguvu katika mapambano dhidi ya uhalifu mtandao na kuelezwa ya kwamba nguvu kubwa itasogezwa mashuleni ili kukuza uelewa wa maswala ya uhalifu mtandao (Awareness) na kusisitizwa hiyo ndio itakua shabaha yao ya awali.Taarifa iliyoandikwa na gazeti la kila siku la nchini humo kupitia tovuti yake.
 
Kupitia program ya mpango uliopewa jina la “Cyber safety pasifika” uliopangwa kuwasaidia watoto, vijana na wakubwa kutumia teknolojia katika hali ya usalama iliyojiri kuanzia mnamo tarehe 19 -25 May mwaka huu (2014) ulilenga kuhakiki matumizi salama ya mitandao visiwani humo unapewa kipaumbele na ukanda mzima wa pasifiki ya kusini kwa ujumla wake.

Makubaliano hayo yalifikiwa wakati wa mkutano ulio fanyika na kuwahusisha wakuu wa polisi wa visiwa hivyo. Kauli mbiu iliyo someka kama “ Historia yetu, Utamaduni wetu na mitandao yetu” Ilidahmiriwa kuhamasisha matumizi salama ya mitandao na simu katika ukanda huo wa pasifiki ya kusini.

Bi. Juanita Matanga
Bi. Juanita Matanga, Mkuu wa polisi wa visiwa hivyo aliainisha utayari wa kujipanga kukabiliana na uhalifu mtandao huku akitolea maelezo ukuaji wa kasi wa matumizi ya mitandao na simu katika visiwa hivyo na duniani kwa ujumla. Aidha Alieleza ukuwaji wa matumizi ya mitandao bahati mbaya wengi hawajui athari zake. Hilo ndilo lililo wasukuma kuanzisha kampeni hiyo ya kukuza uelewa wa maswala ya uhalifu mtandao (Cybercrime Awareness Campaign) visiwani humo.

Matanga alisisitiza kampeni hiyo itakua endelevu na pia kutakua na kupitia sharia zilizopo ili kuweza kuziboresha kuhimili makosa ya uhalifu mtandao. Alianisha pia katika visiwa hivyo bado ukuaji wa kasi wa makosa ya kimtandao haujaanza kuonekana na polisi visiwani humo wako katika kuhakiki wanakuza uelewa kwa raia wake ili kuweza kukabiliana na hali hiyo – Kuzuia tatizo ni bora zaidi kuliko kusubiri tatizo litokee ili kuanza kukabiliana nalo.

Mkuu huyo wa polisi alianisha pia yakua nchi nyingine za ukanda huo wa pasifiki  tayari wamesha kua na taratibu wa kuhamasisha matumizi bora ya mitandao kukabiliana na uhalifu mtandao (Cybercrime awareness programs)  na umefika wakati visiwa hivyo navyo kuingiza taratibu hiyo katika vitendo na kusisitiza tena kua swala hilo litakua  endelevu.
Na:Yusufu Kileo

Popular Posts

Labels