Serikali ya Tanzania imeomba mkopo wa Dola za Marekani milioni 154 ambazo ni takribani shilingi za kitanzania bilioni 246 kwa India kuwezesha ujenzi wa minara ya mawasiliano ya simu katika maeneo yasiyo na huduma hiyo,ambapo sh.bilioni 320 zinatarajiwa kutumika.
Tayari Serikali imeorodhesha maeneo yanayotakiwa kuwekewa minara na gharama zake ikiwa ni hatua ya kuwezesha kuanza utekelezaji wa ujenzi huo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia,January Makamba amesema bungeni jana wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Bukene,Selemani Zedi (CCM) aliyetaka kujua juhudi za Serikali kujenga minara katika sehemu zisizo na mawasiliano,hususani yasiyo na mvuto wa kibiashara.
Makamba pia amesema kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote ulioanzishwa na Wizara hiyo utasaidia kuharakisha kazi hiyo ya upelekaji huduma za mawasiliano.
Takwimu zilizotolewa na jana na Kampuni ya Simu ya Vodacom zinaonesha kwamba Kenya inaongoza kwa mawasiliano ya mawasiliano ya simu na intaneti kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ikifuatiwa na Tanzania,Uganda,Rwanda na Burundi.
Takwimu hizo zinaeleza kuwa julai mwaka jana Kenya yenye wakazi milioni 44,inawatumiaji wa simu za mkononi milioni 34.4 huku intaneti wakiwa ni milioni 16.3 sawa na asilimia 41.
Tanzania inafuata kwa kuwa na wakazi wapatao milioni 48.3 na watumiaji wa simu za mkononi ni milioni 27.4 na wanaotumia intaneti ni milioni 5.31 sawa na asilimia 11 tu
Friday, May 23, 2014
Popular Posts
-
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika,Raia wa Afrika kutoka Congo-DRC Verone Mankou,amezindua simu aina ya smarthphone na k...
-
--> Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Wamiliki wa Blog (TBN),Joachim Mushi akizungumza na waandishi wa habari Ofisa Uhusiano...
-
Wamiliki wa vituo vya utangazaji vya televisheni nchini, wamesema watasitisha kurusha matangazo ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa kutokan...
-
Explore more visuals like this one on the web's largest information design community - Visually .
-
Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania imeeleza kujivunia mabadiliko ya utumiaji wa Teknohama katika utendaji wake wa kazi katika kipindi ...
-
Afrika ni Bara la pili kwa kuwa na idadi kubwa ya watu ambapo inafikia takribani bilioni 1.2 (wengi wao wakiishi mijini) na inatarajiwa kon...
-
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inasheherekea maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake huku yakiwemo mafanikio makubwa d...
-
Mitandao ya kijamii ni mingi sana,ingawa facebook umekuwa maarufu pengine kuliko hata baadhi ya vituo vya redio ama televisheni. K...