Mtu mmoja ambaye alijitambulisha kwa cheo cha Katibu wa Usaili Idara ya Uhamiaji Dr Mawazo Kaburugu anatafutwa na idara hiyo kwa tuhuma za kutoza watu sh 10,000 kwa njia za udanganyifu.
Mtu huyo ambaye alifanikiwa kutuma ujumbe kwa watu zaidi ya 900,wanaotaka kufanyiwa usaili kwenye idara ya Uhamiaji,anadaiwa kupata kiasi kikubwa cha fedha kutokana na ujumbe aliokuwa akutuma kwa watu hao.
Ujumbe huo ulisomeka "Habari ndugu,pongezi kwa kuitwa kwenye usaili kuanzia tar 9/6.Idara ya uhamiaji inakufahamisha kuwa unatakiwa kulipa sh 10,000 na haitarejeshwa kama gharama za usaili vikiwamo vitambulisho pekee ndio wataruhusiwa kuingia ukumbini,malipo yote yatumwe kwa tigo pesa kwenye namba 0715 54 62 81 kuanzia tarehe 26 hadi 30,kisha tuma sms yenye code za Tigopesa na jina lako kamili,imetolewa na Kamishna Dr Mawazo Kaburugu Katibu wa Usaili".
Mwandishi wa gazeri la Raia Tanzania aliwasiliana na mtu huyo ambapo alieleza kuwa wote ambao wameitwa kwenye usaili watume fedha hiyo kama ujumbe ulivyotolewa na kuongeza kuwa pesa hiyo inahitajika haraka sana ili iweze kufanyakazi iliyokusudiwa kwa ajili ya usaili.
Kaimu Mtendaji wa Idara ya Uhamiaji,Tatu Bruani amesema mtu huyo ni tapeli na ambao wametumiwa ujumbe wasitume pesa hizo.
Chanzo:Gazeti la RaiaTanzania
Popular Posts
-
ILI kuboresha utoaji huduma kwa umma hivi karibuni Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeanzisha utaratibu wa kupokea malala...
-
Ted Wilson na mkewe Nancy Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Ulimwenguni Ted N.C. Wilson ameziundua rasmi mawasiliano ...
-
Laini za simu za mitandao ya simu nchini Tanzania ambazo hazijasajiliwa zitazimwa rasmi Julai 10, mwaka huu. Naibu Waz...
-
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA Kufuatana na kifungu nambari 41 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki ...
-
Mtandao wa Facebook umelaumiwa kwa kuwafanyia wateja wake utafiti wa kisaikolojia bila ya kuwajulisha. Nia...