Nchini China kumezuka gumzo baada ya serikali kupiga marufuku matumizi ya Window 8
katika computa zote za serikali nchini humo. Taarifa iliyo chapishwa na “CHINA DAILY” ilibainisha uamuzi huo wa serikali uliowekwa kwenye tovuti ya serikali ya
nchini humu ambapo ilisisitiza zoezi hilo hali husu komputa za watu binafsi
isipokuwa zile zinazotumiwa na serikali.
Tangazo
hilo la serikali linalosemeka “HAPA” limebainisha uamuzi huo wa serikali
umekuja baada ya kufungiwa huduma za kiusalama kwa Window XP huku likiweka wazi
ya kuwa wamefikia hapo kutokana na sababu za kiusalama mtandao. Komputa hizo za
serikali zitakua ziki tumia Operating system nyingine yoyote isipokua Window 8 ilisistizwa.
Kwa
sasa nchini uchina inasemekana Komputa nyingi za serikali zilikua zinatumia
Window Xp ambayo imekua si salama tena kimtandao ambapo inaweza ruhusu mhalifu
kupenya na kuleta madhara kwa mtumiaji hivyo kuongeza wimbi la uhalifu mtandao
kwa sasa, hususan watumiaji wa Window hiyo iliyositishiwa huduma kwa sasa.
Kwa
upande
wa Microsoft, Imeonyehsa mshangao kuwa window 8 imeonywa kutumika
nchini
humo ilhali wanaamini iko salama na wanaipatia huduma zozote za
kiusalama kila inapo hitajika, Msemaji wa Microsoft alinukuliwa akisema
hivyo na kusisitiza ya kuwa
Microsoft imekua ikitumia nguvu ya ziada kuhakiki bidhaa zake na huduma
zake
zinafikia kiwango cha matumizi kwa mujibu wa mahitaji ya serikali.
Uchina
imeonyesha dhamira yake ya kuongeza nguvu katika kutengeneza Operating system
zake zenyewe, huku Bwana Qi Xiangdong, raisi wa Qihoo 360, akieleza ni muda
muafaka kwa makampuni ya nchi hiyo sasa kukuza utengenezaji wa operating system
zake.
Kwa
upande wa balozi wa uchina nchini marekani amesita kutoa kauli ya haraka
ikizingatiwa kuwepo na hali isiyo njema inayo husiana na maswala ya kiusalama
mtandao kwa nchi hizo mbili ( Marekani na Uchina)