Saturday, May 3, 2014

HALMASHAURI YA KINONDONI YANUFAIKA NA ULIPAJI WA KODI KWA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI NA MAX-MALIPO

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeleza kuwa imenufaika na utaratibu mpya wa utaratibu wa ulipaji wa kodi kwa kutumia huduma ya simu za mkononi na Max-malipo.

Taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Kinondoni Sebastian Modestus Mhowera imeeleza kuwa huduma hiyo mpya inayotolewa kupitia mfumo unaojulikana kama “e–payment system”,ambao unamwezesha mwananchi kulipa kodi yake muda wowote, kwa haraka na urahisi na mahali popote.

Huduma hii inatolewa na Manispaa kwa kushirikiana na wakala anayetambulika kama “Max-malipo” ambaye kupitia huduma zake mitaa 171 iliyopo katika Kata 34 imeunganishwa katika mifumo hiyo ya ulipaji kodi.


Mfumo huu wa ukusanyaji wa kodi ndani ya Manispaa ni hatua ya utekelezaji unaozingatia maelekezo ya waraka wa Serikali Na. 5 wa mwaka 2009 unaohamasisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEKNOHAMA) kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma kwa Umma, kwa ufanisi na kwa wakati.
 

Taarifa inaeleza kuwa manispaa hiyo iliona ni vema ikaingia katika utaratibu huu ili mwananchi aweze kulipia kodi popote kwa kutumia Max-malipo au wakala wa simu za mkononi yaani Tigo pesa Na. 212888 na M-Pesa Na. 212888.

Katika kipindi kifupi cha muda wa miezi 3, tangu mfumo huu mpya ulipoanzishwa rasmi kumekuwa na

• Ongezeko la ada ya kuchangia huduma za Afya (Cost sharing) imeongezeka kutoka Tshs. 45,000,000/= kwa wiki hadi kufikia Tshs. 65,000,000/= kwa wiki, sawa na ongezeko la 69%

• Chanzo cha kodi ya majengo hadi mwishoni mwa Machi zilikusanywa Tshs. 339,000,000/= tofauti na awali ambapo hadi kipindi kama mwaka 2013 zilikuwa kwa  ongezeko la asilimia 269 hiki Tshs. 126,000,000/=

• Maeneo mengine ongezeko la mapato limezidi bajeti ya mwaka iliyotakiwa kukusanywa. Kwa mfano katika ushuru wa huduma za jiji (City Service Kavy) ambapo tumezidi kwa 18%

• Ushuru wa Masoko umeongezeka kwa wastani wa asilimia 20 ya lengo la kila mwezi.

• Lesseni za biashara hadi Machi zilikusanywa shs. 2.4 Bilioni sawa na 93% ya bajeti ya Manispaa ya chanzo hiki ya shilingi. 2.6 Bilioni kwa mwaka.



Popular Posts

Labels