Mwishoni mwa juma lililopita pamegundulika hali mbaya ya kiusalama mtandao itakayo waathiri watumiaji wa kivinjari kijulikanacho kama "internet explorer" ambapo watumiaji wa kivinjari hicho wako hatarini kuweza kuingiliwa kirahisi computer zao na wahalifu mtandao.
Jumamosi iliyopita tangazo hilo linalosomeka hapa "TANGAZO"
limeweza kubainisha internet explorer toleo la sita (6) hadi la kumi
na moja (11) yote yameweza kugundulika yanatoa mwanya kwa wahalifu
mtandao kupenya kwa watumiaji na kuchukua taarifa zozote zitakazo
patikana kwenye computer zao.
Aidha,
Kampuni inayojihusisha na na maswala ya ulinzi mtandao ya "FireEye"
imeonyesha takwimu yakua asilimia 56 ya vivinjari, hadi ilipofikia
mwaka 2013 vilikua hatarini kuingiliwa na wahalifu. Na kubainisha kwamba
wahalifu wamekua na uwezo wa kutengeneza vivinjari visivyo sahihi
vinavyo weza ruhusu wahalifu hao kuingilia computer za watu mara tu
watumiaji wa vi vinjari hivyo wanapo vitumia.
Microsofti imeshindwa kupata suluhu ya tatizo hilo ambapo CERT ya marekani imetoa tahadhari inalosomeka hapa "CERT ALERT"
yakuwa watumiaji vivinjari vya "internet explorer" wanapaswa kubadili
vivinjari kwa sasa na badala yake watumie vingine kama vile (Mozilla
fox, Google chrome n.k) hadi hapo tatizo litakapo rekebishwa na
kutangazwa vingenevyo.
Aidha,Christian Tripputi Ametumia muda huu kuonya watumiaji wa Window XP yakuwa kwa sasa wako hatarini kwani hakuna tena huduma zitakazo endelea kutolewa kwa Window hiyo na wahalifu mtandao wamesha anza kuleta madhara kwa wote wanaoendelea na matumizi ya windo hiyo na kusisistiza hapata kuwa na msaada kwa waathirika.
Taarifa ya kingereza inasomeka inapatikana hapa