Uongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Magomeni Mwembechai umewataka washiriki wa
kanisa hilo kutumia taasis za kibenki na mifumo ya kuhamisha pesa kwa njia ya
mitandao ya simu katika utoaji wa sadaka na michango ya kanisa ili kuepukana na
uhalifu wa fedha.
Usiku wa
kuamkia April 24,mwaka huu kati ya saa 9 hadi saa 10 alifajiri watu
wanaodhaniwa kuwa ni majambazi walivamia Kanisa la Waadventista Wa Sabato
Magomeni Mwembechai na kupora kasha la fedha,projekta moja ,nyalaka muhimu za
kanisa na kufanya uharibifu wa ofisi ya mchungani wa kanisa hilo.
Akitoa
taarifa ya uongozi wa kanisa kwa washiriki siku ya sabato,Mzee Kiongozi wa
Kanisa la Waadventista Wa Sabato Magomeni Mwembechai,Msafiri Mbibo amesema
imefikia wakati sasa kwa washiriki kutumia mifumo ya kisasa ya mitandao ya simu
katika utoaji wa sadaka ama michango ambayo itakuwa ikiwekwa kwenye taasisi za
kibenki moja kwa moja ili kuepusha uhalifu kanisani hapo.
Taarifa hiyo
ilieleza kuwa kanisa hilo lina mfumo wa utunzaji wa taarifa za kifedha wa
teknolojia ya habari na mawasiliano ambao haukuathiriwa na uharibifu uliotokea
kanisani hapo.
Kanisa la
Waadventista Wa Sabato Magomeni Mwembechai lilijengwa mwaka 1963,na sasa liko
katika mchakato wa ujenzi wa kanisa kubwa
linalokadiriwa kugharimu takribani shilingi bilioni 3 za kitanzania.