Tanzania iko katika hatua muhimu ya
utekelezaji wa mfumo wa kompyuta katika utoaji wa mizigo(National Electronic Single Window System) katika bandari,
majabio ya mfumo huu yataanza mwezi Juni 2014, ili kurahisisha ufanyaji
biashara na kuchangia kuinua uchumi wa Tanzania.
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Bandari Phares Magesa amesema Mradi huo unasimamiwa na
Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa niaba ya wadau wote na utanufaisha
watumiaji wa bandari zote, viwanja vya ndege, mipaka yote ya
Tanzania. Mfumo huu unatarajiwa kupunguza muda wa mizigo kukaa bandarini
na hivyo bidhaa kuingia katika mzunguko wa uchumi haraka.
Wadau
wa Port Community System wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
kikao mapema juma hili.
Mwenyekiti
wa wadau Ndg. Igogo kulia akijadiliana jambo na Ndg. Magesa kwa niaba ya wadau wote wa Bandari, kushoto ni
Meneja Mkuu wa kampuni ya Phaeros Group ya Ubelgiji ambao ndio
watengenezaji wa mfumo huo.