Friday, April 25, 2014

MTANDAO WA TIGO KUTOA HUDUMA YA FACEBOOK KWA LUGHA YA KISWAHILI


Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania Diego Gutierrez (Kushoto) akipongezana na  Mkurugenzi wa Ushirikiano na Ukuaji wa Kimataifa wa Facebook Nicola D'Eli baada ya kuzindua huduma ya Facebook bila malipo kwa lugha ya kiswahili kupitia mtandao wa Tigo (Picha na Tigo Tanzania)

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Tanzania imezindua mpango wa kutoa bure huduma za mtandao wa kijamii wa Facebook kwa lugha ya kiswahili .

Huduma hiyo inatolewa kwa mara ya kwanza,itawanufaisha wateja wake waote nchini Tanzania na wale wa nchi zingine za Afrika Mashariki.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Dar es salaam jana,Mkurugenzi Mkuu wa Tigo,Diego Gutierrez alisema ushirikiano huo utawawezesha wateja wanaotumia mtandao wa Tigo kuperuzi kwenye facebook kupitia simu zao za mkononi bila gharama zozote na kwa lugha ya kiswahili badala ya kiingereza.

Tanzania itakuwa ni nchi ya Pili kupata nafasi ya kuzinduliwa kwa huduma hiyo,Paraguay ilikuwa ya kwanza kupata huduma sawia na hiyo ambayo ilizinduliwa Desemba mwaka jana na watumiaji wa mtandao huo wanatumia lugha ya Kiguarani.

Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya watu wanaotumia mtandao wa Facebook nchini Tanzania ni milioni 2 ,huku kukiwa na idadi ya watumiaji wa mtandao huo bilioni 1.2 duniani.

Popular Posts

Labels