Mamlaka
ya mawasiliano Tanzania (TCRA) inatarajia kuzima rasmi mitambo ya
analojia ya urushaji wa matangazo ya televisheni katika miji ya Bukoba mkoani Kagera na Musoma,Mara mwishoni
mwa mwezi huu.
Naibu
Mkurugenzi Idara ya Utangazaji wa Mamlaka hiyo,Frederick Ntobi amesema
zoezi hilo la uzimaji wa mitambo hiyo na kuhamia dijitali katika miji
hiyo litaendeshwa saa 6:00 usiku.
Kwa mujibu wa Ntobi,zoezi hilo litahusisha mitambo inayotumia mfumo wa satelaiti,matangazo kwa njia ya waya au mitambo ya radio.
Amesema
uzimaji wa mitambo hiyo ni awamu ya pili baada ya kwanza kuhusisha
mikoa ya Dar es salaam,Mbeya,Tanga,Mwanza,Arusha na Mbeya.
Aliwataka
wakazi wa wilaya hizo za Bukoba na Musoma kuhakikisha wananunua
ving'amuzi ili waweze kuangalia vipindi mbalimbali vya kwenye
televisheni.
Popular Posts
-
Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL) jana imekabidhi mradi wa mawasiliano utaotumiwa katika mikoa 12 ya Tanzania kwa ofisi ya Mkaguzi na ...
-
Miaka michache iliyopita kulikuwa na changamoto ya kuhifadhi vitu sehemu ambayo mtu anaweza kutumia akiwa popote duniani akiwa ame...
-
Ofisa Biashara wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Thomas Lemunge akitoa ufafanuzi katika semina kwa wahariri juu ya mkongo wa taifa katika...