Tuesday, April 1, 2014

MASWALI NA MAJIBU KUHUSU KUVURUGA PROGRAMU YA WINXP

MASWALI NA MAJIBU KUHUSU KUVURUGA PROGRAMU YA WINXP

1 – PROGRAMU YA WIN XP KUVURUGIKA 
Sio ukweli kwamba programu ya win xp itavuruguka kama inavyoelezwa na watu wengi .
2 – KITAKACHOTOKEA 
Microsoft itaacha kutoa baadhi ya huduma za kuboresha windows xp kwa jina lingine ni updates ambazo zilikuwa zinapatikana pale mtu anapojiunga kwenye mtandao bure .
Unapokosa hizi updates maana yake windows xp yako inakuwa haikostable kupambana na mengine yanayoweza kutokea kwenye kompyuta yako haswa upande wa software , kwahiyo updates ni sawa na mtu anavyokula chakula kunachoenda kuboresha afya yake aweze kuendelea kuishi na kufanya shuguli nyingine .

3 – VIPI PROGRAMU NYINGINE 
Kampuni nyingi za program zimeboresha na zinaendelea kuboresha program zao ili ziweze kufanya kazi na operating system mpya za zilizoboreshwa zaidi kama windows 7 , 8 , 8.1 ETC .

Mfano sasa hivi kuna printa ambazo hazina program za win xp kwahiyo ukiwa na win xp huwezi kutumia printa hizo .

4- KWA WANAOENDELEA KUTUMIA WINDOWS XP
Kama nilivyoeleza Microsoft haitokuwa inatoa msaada na updates za kuboresha windows xp , ili uhamie windows 7 , 8 na nyingine zilizokuwepo katika matumizi , hii ina maanisha Microsoft haitahusika na suala lolote la kisheria litakalotokea endapo utaendelea kutumia .

5 – WENGINE WAMEFANYAJE ?
Kuna baadhi ya kampuni zimeingia mkataba na Microsoft kwa ajili ya kuendelea kuhudumia windows xp zao huku wao wakiendelea kufanya mchakato wa mabadiliko kidogo kidogo kulingana na uwezo wao wa kifedha na sera za kampuni , sherika au nchi husika , kwa Tanzania watu wangejaribu kuwasiliana na ofisi za Microsoft nchini Kenya hawa wanaweza kuwapa msaada zaidi haswa kwa mabenki na huduma nyingine kubwa kubwa .

6 – TATIZO LA AFRIKA NA NCHI MASIKINI 
Hizi program za windows xp , windows 8 na 7 ni gharama sana , kwa mfano windows 7 kwa Tanzania ni dola 250 hivi ukichanganya na office unapata dola 500 ukiweka na antivirus ni dola 550 hiyo ni kama ukiamua kununua genuine na DVD zake , hii watu wengi hawana uwezo wa kununua na hizi serikali zetu na uwezo wao ni mdogo , kuwapeleka huko juu ni gharama zaidi kwa watu na serikali .

USHAURI WANGU 
Serikali iingie mikataba na kampuni zinazouza program zao kwa wingi nchini Tanzania haswa Microsoft , adobe , apple , kaspersky , Symantec , oracle , ETC ili waweze kufanya mipango ya kupunguza bei kwa ajili ya soko la Tanzania hii itasaidia watu kupata program halisi kwa bei nzuri kidogo na zenye uhakika bila hivyo wananchi watakimbilia kwenye program ambazo sio halisi na wataendelea kutumia gharama kubwa kwenye matengenezo na kukumbana na karaha nyingine za kihalifu .

YONA F MARO 
O786 806028

Popular Posts

Labels