Saturday, April 5, 2014

KWANINI UNAHITAJI UPDATES ZA KOMPYUTA/SIMU?


Watu wa TEKINOHAMA haswa wanaohusika na masuala ya Ufundi au kusimamia masuala ya usalama huwa wanaulizwa maswali 2 sana .

Hivi naweza kutumia Kompyuta yangu bila kufanya updates ?

Naweza kupata Antivirus ambayo hainiulizi/Haitaki updates ?

UPDATES KATIKA KOMPYUTA/SIMU NI NINI ?

Updates ni zile programu zinazoingizwa au ingia kwenye kompyuta yako au simu yako kwa ajili ya kuboresha programu za kompyuta yako au simu yako .

Kama ulinunua kompyuta ikawa na programu inayoitwa UJAMAA 1.2 , Baada ya mwaka au miezi kukiwa na UJAMAA 1.3 basi hii ndio update ya toleo 1.2 , update hii unaweza kuipata bure au kulipia kulingana na Kampuni yenyewe lakini update nyingi ni bure .
Kuweka updates ni sawa na mwanadamu anavyokula vyakula ili aweze apate afya aweze kuendelea kuishi na kufanya shuguli zake mbalimbali za kujipatia kipato .

UPDATES ZINAPATIKANAJE ?

Kuna njia 2 za kupate updates :-

1 - Kwa Njia ya Mtandao( Moja Kwa moja ) - Hii inatumika kama kifaa chako kimeunganishwa kwenye mtandao na umekiruhusu kupokea updates kwa njia za mtandao , mara nyingi updates hizi kufanya moja kwa moja ikimaliza inaingiza yenyewe kwa kuinstall .
Njia hii inakuunganisha moja kwa moja na mtengenezaji wa programu husika .

2 - Kwa Njia ya Download - Hii ni kwa watu wasiokuwa na huduma ya mtandao lakini wanataka kupata update fulani au wakati mwingine mtu shirika lina kompyuta 200 na zote wanataka kuweka update moja lakini bila kuunganisha kwenye mtandao , unachofanya ni kwenda kwenye tovuti husika ya programu utapata update hiyo na utapata maelezo ya jinsi ya kuitumia .

Hii unaweza kufanya hata kwenye internet cafe yenye kompyuta nyingi au ofisi zenye kompyuta nyingi kwa kudownload file moja ambalo utaweza kutumia kwenye zote .

3 - PATCH - Hizi ni updates pia lakini lengo lake haswa ni kurekebisha kosa ambalo lilifanyika wakati wa utengenezaji wa programu hisika , hii nayo ni bure kwa programu nyingi .

4- Plugins - Hivi ni viongo/Viongezeo katika programu mbalimbali za kompyuta au simu kwa ajili ya kuboresha utendaji wa kitu fulani , hizi zinatumika zaidi kwa watu wa uhandisi na uchoraji au uchanganyaji picha , utakuta kuna kitu anahitaji kufanya kutumia programu yake badala ya kuwa na programu fulani kubwa basi ataweza kupata Plugin moja ndogo ya kufanya kitu hicho specific .

Tafadhali usitumie Plugin kama hujui unachofanya ni rahisi kukuharibia mambo yako

UPDATE HUFANYIKA BAADA YA MUDA GANI ?

Kila kampuni inayotengeneza bidhaa ina sera zake kuhusu updates lakini kila zinapotoka huwa kwenye mtandao wa kampuni husika kama ulikosa unaweza kutafuta ukapata lakini kama umenunua kompyuta leo au simu ukijiunga tu utalazimika kupata updates zote zilizopita mpaka leo vile vile kwa antivirus na Simu .

Mara nyingi
Zaidi unaweza kufuatilia vyombo vya habari na kusoma kwenye mitandao kama kuna updates zozote kuhusu programu husika .

MUHIMU

Kompyuta nyingi zenye programu ambazo sio halali wanaogopa kufanya updates kwa hofu kwamba atakamatwa au itafanya hili na lile , bora upate ujumbe kwamba unatumia programu bandia na uendelee kuitumia kuliko kutokufanya updates kabisa kwa sababu utakuwa unabadilisha mafundi kila siku na itakuwa rahisi kwa kifaa chako kushambuliwa au watu kutumia kama mlango wa kufanya mashambulizi kwenye mitandao mingine .

Kama mko maofisini au majumbani ni vizuri muwe na sheria kali kuhusu kufanya updates za vitu mbalimbali vinavyotumia programu maana itakuwa nafuu na ulinzi tosha kwako na kwa mali zako .

Kuna watu wanaibiwa data zako kwenye kompyuta kwa sababu tu hakufanya updates kwenye antivirus yake matokeo yake alipoingia kwenye kompyuta spyware wakaingia wakaweza kutumiwa kuhamisha taarifa au mambo mengine .
YONA F MARO
0786 806028
 

Popular Posts

Labels