Kumetokea matukio kadhaa ya wizi kwa njia ya mtandao
unaohusisha simu za mikononi katika utoaji wa fedha ingawa pesa nyingi
zimetolewa kwa ushirikiano wa wafanyakazi wa kampuni za simu .
Tukio kubwa sana ni lile la kampuni moja kupoteza karibu bil
2.5 kwa mkupuo , ambapo walihusika wafanyakazi zaidi ya 5 huku mmoja wao akiwa
ameacha kazi kabla ya tukio nitaeleza tukio hili kwa ufupi .
Hii kampuni haina tabia ya ufanya utaratibu wa kufuta rekodi
za mtu aliyeacha kazi ndani ya muda mfupi haswa zile taarifa zake za kuingia
kwenye kompyuta au anapotaka kuingia kwenye database na program nyingine za
kiofisi .
Kilichotokea huyu kijana alivyoacha kazi , wenzake wakajua
hivyo walijua kuna taarifa Fulani zimeachwa kwahiyo wakafanya utaratibu wa
kufanya recovery ya password za huyu kijana aliyeacha kazi .
Password zilipatikana zote kwa ushirikiano wa kijana mwingine
wa kitengo cha Tehama , kwahiyo wakaingia kwenye kompyuta ya huyu kijana
aliyeacha kazi na kutengeneza wakala feki wa kutoa fedha , wakafungua zaidi ya
10 halafu wakaweka watu wao .
Wakaanza kutoa fedha kupitia hao wakala feki , kilichofanya
washtukiwe ni kitendo cha kutaka kuhamisha zaidi ya mil 400 kwenda kwenye
akaunti ya mmoja wao ndio hapo benki walipopiga simu kwenye kampuni hiyo ili
kupata taarifa zaidi kwa bahati nzuri alipokea mtu wao , kesho yake benki
ikapiga tena ndipo mwenzao hakuwepo , ndipo mchezo wao uliishia hapo
walikamatwa lakini sasa wako nje sijui kesi yao iliishia wapi .
……………………………………………………………………………… ………..
Siku nyingine mfanyakazi mmoja wa kampuni ya simu alienda kwa
dada mmoja kuomba namba yake ya uwakala akamwambia atamwingizia hela kiasi cha
mil 1 kila siku kwa siku 3 yeye achukue laki 3 kwa kila hamisho .
Huyu mfanyakazi aliwasiliana na mawakala zaidi ya 50 kwa
makubaliano hayo , kumbe huyu mfanyakazi alikuwa anafanya taratibu za kuacha
kazi na kweli aliacha kazi akaenda kufuata zile fedha .
Kampuni ya simu ikashtuka hela zimehamishwa kwenda kwa
mawakala hao na mfanyakazi ameacha kazi , walikuwa wameshachelewa sana ,
waliopata shida ni mawakala kwa kufungiwa huduma zao wengine kupelekwa polisi .
……………………………………………………………………………… ……..
Ukiwa unatoa huduma za uwakala wa kutoa fedha basi usipende
kuzoeana sana na watu , kama unapenda sikiliza kisa hiki .
Mtu mmoja alizoeana na wakala Fulani kiasi kwamba aliweza
kujua hata bosa wa yule wakala majina yake na namba zake za simu na hata vitu
vingingine vidogo vidogo .
Siku moja huyu jamaa kwa kutumia program ya kompyuta
akamwandikia huyu wakala sms . NAOMBA UTUME KIASI CHA LAKI 4 KWENYE NO 98686
JINA LAKE NI SSSS .Wakala kuangalia namba ni ya bosi wake kweli hakutaka
kuhakiki hiyo sms vizuri yeye akahamisha hela akaibiwa .
Siku ya pili huyu mhalifu alienda kwa mtu mwingine kwa
kutumia hiyo program akaandika ujumbe wa kutoa fedha kiasi cha laki 4 ,wakala kuona sms akajua
kweli yule mtu katoa hela kampa mhalifu hela kumbe ile ilikuwa sms tu , siku
nyingine akajifunza mtu akitoa hela hakikisha nae anapokea sms ya kuthibitisha
kutoa hela .
ITAENDELEA SIKU NYINGINE .
YONA F MARO