Serikali ya Tanzania imesema inatoza kodi ya shilingi 1,000 kwa
mwezi kwa kila laini yenye namba ya simu.Umoja wa Makampuni ya mitandao ya simu
Tanzania (MOAT)umeeleza kuwa makato hayo ya kodi yameanza rasmi julai 1 mwaka
huu.
Takwimu zinaeleza kuwa
matumizi ya simu za mkononi nchini Tanzania yamefikia asilimia 48,ambayo ni sawa na watumiaji
milioni 22 wa simu za mikononi katika
nchi hiyo yenye wakazi wapatao milioni 44 ambapo miongoni mwao milioni 8
hutumia chini ya shilingi 1,000 za Tanzania kwa simu zao kwa mwezi.
MOAT imeeleza kuwa japokuwa inafahamu kuwa serikali
inahitaji kuongeza mapato kwa ajili ya kuondoa umaskini kodi hiyo ya laini za simu kwa mwezi
itawathiri maskini na soko la simu kwa ujumla.
Umoja huo umeiomba
serikali kutazama upya uamuzi huo ili kukuza maendeleo ya mawasiliano ya simu
nchini Tanzania.
chanzo:telecompaper
chanzo:telecompaper