Kuwa na Akaunti ya Facebook ni kwa manufaa yako na manufaa ya Facebook |
Facebook ambayo kwa sasa inapatikana
katika lugha 70 ulimwenguni, ni mtandao wa jamii ambao unaongoza kwa kuwa na
watumiaji wengi zaidi duniani. Wewe na mie kama watumiaji wa Facebook
tunainufaisha kampuni hiyo ya Facebook, kwani kupitia kuitumia kwetu
kunaiwezesha Facebook kuingiza mapato kwa njia ya moja kwa moja au nyingine.
Makala hii inakuchambulia namna
ambavyo Facebook inaingiza "vijisenti" vyake:-
1. Kupitia Matangazo: Kwakuwa inao watumiaji wa mtandao wengi, ni rahisi kwa
Facebook kushawishi watu binafsi na makampuni kutangaza bidhaa zao kupitia aina
mbalimbali za matangazo yanayorushwa hewani na Facebook. Mfano , kampuni
inaweza kudhamini POST yake, ili ionekane kwa watu wengi zaidi na mara nyingi.
Pia kuna matangazo ya biashara ambapo unaweza kutengeneza tangazo lako la
biashara na kulirusha hewani kupitia Ukurasa wako wa Facebook (Facebook
Page). Ili kutengeneza tangazo Facebook, unaweza kuenda sehemu maalum
ukiwa Facebook imeandika
CREATE AN AD.Unahitaji kuwa na Credit Card au
Umejisajili na unayo akaunti ya Paypal ili kuweza kulipia
huduma hii.
Mfano wa Matangazo yanayoipatia fedha facebook |
2. Salio maalum la Facebook (
Facebook Credit)
Ni kama vile unavyonunua salio la
simu yako ili utumie salio hilo kupiga simu, ila kwa Facebook, unaponunua Facebook Credit, ni kwa ajili ya kuweza kutumia
credit hiyo kulipia kucheza Games, au hata kununua vitu katika baadhi ya maduka
yanayouza bidhaa zao ndani ya Facebook.
Unahitaji kuwa na Credit Card au
Umejisajili na unayo akaunti ya Paypal ili kuweza kununua
Facebook Credit.
3. Kupitia Kuuza bidhaa mbalimbali
Facebook inayo huduma ya kuuza
bidhaa mbalimbali kwa mtindo wa "Gift" ambapo wewe mtumiaji unachagua
nani unataka kumnunulia bidhaa , kisha unaenda kwa profile ya huyo unayetaka
kumuuzia bidhaa. Utaona sehemu imeandikwa GIVE GIFT, ukibofya hapo utakutana na
aina mbalimbali za zawadi na maelekezo. Hata hivyo huduma hii ya kutoa zawadi
kwa watu haipataki kwa kila nchi. Inabidi ucheki Profile ya mtu husika
unayetaka kumpa zawadi kuona kama GIVE GIFT ipo katika profile yake.
Chanzo:Mbuke Times Blog