Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania imesema kuwa imeshazima laini za simu 200,000 ikiwa ni utekelezaji wa sheria ya posta na mawasiliano ya kielektroniki ya mwaka 2010 ikimbatana na muda wa mwisho wa kusajili laini za simu nchini Tanzania kuwa ni julai 10,2013 uliowekwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Usimamizi wa Sheria wa Airtel Tanzania Beatrice Singano amesema waliwajulisha wateja wao mapema kusajili laini zao za simu ili kuepuka kufungwa kwa laini za wateja wao.
Amesema kuanzia julai 10 mwaka huu kama mamlaka ya mawasiliano Tanzania ilivyotangaza Aprili mwaka huu kwa sasa jumla ya wateja 200,000 wa kampuni hiyo wamefungiwa laini zao kutokana na kutosajili.
Ili kufahamu laini ya simu imesajili mmiliki wa simu anapaswa kuhakiki usajili huo kwa kupiga *106#.
Usajili wa namba za simu kama ilivyo katika nchi mbalimbali duniani umekuwa ukiendelea na kwa miaka michache katika nchi za Afrika Mashariki lengo likiwa ni kudhibiti matukio ya uharifu yanayofanywa ama kuanzishwa na watumiaji wa simu za mikononi katika nchi hizo.
Popular Posts
-
Benki ya CRDB imewaonya wateja wake kuwa makini na baadhi ya mitandao inayoibuka na kulaghai kwa kuwataka wananchi,kutoa taarifa zao muhimu ...
-
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akizungumza kabla ya kuzindua rasmi maonesho ya Tehama yanayoend...
-
Laini za simu za mitandao ya simu nchini Tanzania ambazo hazijasajiliwa zitazimwa rasmi Julai 10, mwaka huu. Naibu Waz...
-
Kampuni ya magari ya Fiat Chrysler kutoka Marekani imeyarudisha magari yake yapatayo milioni 1.4 baada ya watafiti wa usalama kuony...
-
Watumiaji wa programu ya komputa iitwayo Window XP wamepewa tahadhari na kampuni ya Microsoft ambayo ndiyo iliyotengeneza program hiyo ...