Na Brown Nyanza
Wanasayansi
wawili katika nchi ya Ujerumani wamegundua kalamu inayotoa alama pindi mwandishi
anapokosea herufi “spelling error.” Kalamu hiyo imepewa jina la Lernstift neno la kijerumani linalomaanisha
learning pen, Yaani kalamu ya kusomea ama kujifunzia
Katika mahojiano maalumu katika kituo cha CNN, Mmoja ya Wanasayansi hao alisema
wazo la kalamu hiyo limekuja baada ya kuona mke wake akikasirika mara kwa mara pindi
anapomuona mtoto wao akihangaika kwa kukosea herufi kila mara wakati
wa kufanya mazoezi ya nyumbani (homework),
Ndipo akasema kwa hasira “kwanini kusiwe na peni inayotoa alama fulani pindi mtoto anapokosea
herufi wakati wa kuandika.” Ndipo mawazo ya mumewe yakaenda mbali zaidi na
kufikiria kuteneneza peni hiyo iliyoleta gumzo kubwa duniani.
Kalamu hiyo hutoa
alama kwa kutetemeka “vibration” pindi unapokosea herufi wakati wa kuandika.
Kwa sasa kalamu
hiyo inagundua lugha mbili tuu, kingereza na kijerumani, pia unaweza
kuunganisha na Smartphone yako, tabiti au computer na kuona kitu unachokiandika
katika karakasi.
Chanzo: CNN