Serikali nchini Tanzania imetakiwa kuimarisha
kitengo cha upelelezi na ufatiliaji wa makosa jinai yanayofanywa kupitia
mitandao ya simu za mkononi na intaneti.
Rai hiyo imetolewa na wamiliki, wafanya
kazi na mawakala wa makampuni ya kutuma na kusafirisha fedha jijini mwanza yaani tigo pesa, M pesa, airtel
money, na mashirika mengine ambapo wameiomba serikali kuunda kamati ya upelelezi na wataalamu wa kuchunguza mienendo ya watu wanao tumia simu
za mkononi na intaneti kutapeli wananchi mamillioni ya pesa.
Mmoja kati ya wafanyakazi wa makampuni hayo Iyuko
Kiyumba amesema kuwa vituo vingi vya
polisi jijini Mwanza havina wapelelezi
wala wajuzi wanao weza kufuatilia ipasavyo wezi wanao tumia njia za mitando hivyo watuhumiwa wanapo kamatwa huachwa huru
baada ya kutoa ushahidi na mahakama
kukosa nguvu ya kuwatia hatiani watu hawa.
Taarifa zilizotolewa na wamiliki wa makampuni
hayo zimedai kuwa baadhi ya wezi wamesajili laini hizo kwa majina ya viongozi wa
serikali ambapo huzitumia kuwaibia
maafisa wakubwa wa ngazi za juu na wananchi mbalimbali kwa kutumia njia za
kimtandao.