Mswada ambao ungezuia ukusanyaji wa
data za simu unaofanywa na shirika la
usalama wa taifa nchini Marekani , NSA, umezuiwa
na wabunge mjini Washington.
Kura hiyo katika baraza la Seneti
ilikuwa kura 58 za ndio na 42 za
hapana , ikiwa ni kura mbili chini ya kura
60 zinazohitajiwa kuupitisha mswada huo.
Mswada huo uliokataliwa ungefikisha mwisho
ukusanyaji wa data za simu za mamilioni
ya Wamarekani.
Wanaoupinga wanasema ukusanyaji
wa data ni muhimu kwa ajili ya
juhudi za kupambana na ugaidi.
Kiwango cha udukuzi huo ulikuwa
miongoni mwa ufichuaji uliofanywa na mfanyakazi
wa zamani wa shirika la NSA Edward Snowden.