Tuesday, November 11, 2014

WAMILIKI WA BLOG TANZANIA WATAKIWA KUFUATA MAADILI YA UANDISHI WA HABARI




Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo nchini Tanzania Assah Mwambene

Mhandisi wa TCRA,Andrew Kisaka akiwasilisha Mada kuhusu maadili ya Uandishi  na Utangazaji  wa Habari

Wamiliki wa blog mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo


Kamati ya muda ya wamiliki wa blog iliyochaguliwa leo

Mwenyekiti wa Kamati ya wamiliki wa blog Joachim Mushi
Serikali imewataka wamiliki na waandishi wa blog nchini kuzingatia maadili ya taaluma ya uandishi wa habari wakati wa mchakato wa kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi ujao na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Akizungumza jijini Dar es salaam hii leo wakati wa ufungaji wa mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Wamiliki wa blog mbalimbali nchini Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Tanzania Assah Mwambene amesema serikali inatambua blog zinafanya kazi ya kutoa habari sawa na vyombo vingine vya habari lakini vinapaswa kuzingatia uandishi wa mambo ya msingi kwa kufuata maadili ya uandishi wa habari.

Mwambene ambaye pia ni Msemaji wa serikali ameeleza kuwa lazima wamiliki na waandishi wa blog wajue wamechukua wajibu mkubwa unaoendana na wajibu wa kuwajibika kwa wananchi wanaowandikia habari wa kuzingatia maadili.


Awali akizungumza kwenye mkutano huo Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA Habbi Gunze amesema waandishi na wamiliki wa blog wananafasi ya kusaidia umma kuweza kuelewa masuala mbalimbali ya uchaguzi pasipo upendeleo wowote wala uchochezi.


Kumekua na malalamiko toka kwa  wananchi kutokana na habari mbalimbali zinazoandikwa kwenye baadhi ya blog kwa kutozingatia maadili ya uandishi wa habari na utamaduni wa mtanzania jambo ambalo ni changamoto kwa serikali kutokana na uhuru uliopo kwa wamiliki wa blogi hizo na ukosefu wa sheria zinazowaongoza.

Popular Posts

Labels