Watu sita wanaosadikiwa kuwa ni matapeli kwa
njia ya mtandao wa simu wamekamatwa jijini mwanza baada ya kufanya utapeli kwa
watu mbali mbali kwa njia ya simu huku
wakitumia majina ya watu maarufu jijini humo.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa
polisi jijini Mwanza Valentino Mlohola amesema kuwa, November 5 mwaka huu
kijana mmoja anayejulikana kwa jina la Eradius Christian alisajili namba ya
simu kwa jina linalofanana na jina la kamanda huyo.
Kamanda huyo amesema kuwa watu hao wamekuwa
wakisajili majina yanayofanana na viongozi mbali mbali wa serikali na
kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa njia ya simu kitu ambacho ni kosa
kisheria na watu hao wamefikishwa kituo cha polisi na upelelezi ukikamilika
watafikishwa mahakamani.