Kwa
mara ya kwanza, wanafunzi Tanzania wanaweza kujipatia nyenzo za
kujifunzia masomo ya sekondari bila gharama yoyote kupitia mpango wa
Facebook wa Internet.org.
Mfumo
wa masomo ya dijitali wa Shule Direct ni mpango wa kwanza wa aina yake
Tanzania, mfumo huu unawapatia wanafunzi na walimu nyenzo za masomo
zenye ubora wa hali ya juu zilizotengenezwa kufuata mfumo wa elimu ya
Sekondari ya Tanzania.
Watengenezaji
wa nyenzo zinazopatikana Shule Direct ni mabingwa katika fani ya elimu,
hii inahakikisha kuwa nyenzo zipatikanazo Shule Direct ni sahihi,
zinapitiwa na kuhakikiwa mara kwa mara kwa ajili ya maboresho, hivyo
zina ubora wa hali ya juu.
Mfumo
wa masomo wa kidigitali wa Shule Direct unampa mwanafunzi uhuru wa
kujisomea, kujadiliana na kubadilishana mawazo na wanafunzi wenzake
wakati wowote na mahali popote.
Kupitia
Shule Direct wanafunzi wanaweza kujisomea matini (“notes”), kujibu
maswali ya majaribio, pia wanaweza kushiriki mijadala mbali mbali na
wanafunzi wenzao na walimu. Mijadala hii inasimamiwa na msimamizi kutoka
Shule Direct kuhakiki matumizi salama ya mtandao wa Intaneti na kuwa
haki za wanafunzi na watu chini ya umri wa miaka 18 zinahifadhiwa.
Ushirikiano
wa Shule Direct na Internet.org ni hatua madhubuti katika kuhakikisha
teknolojia iliyopo inatumika kuboresha elimu Tanzania. Ushirikiano huu
umekuja wakati muafaka, na ni faida kubwa kwa Shule Direct kwa vile kwa
mpango huu nyenzo zetu sasa zitawafikia wanafunzi wengi zaidi.
Internet.org
ni mpango wa Facebook ambao unalenga kuwezesha watu wengi zaidi ambao
hawana namba ya kuunganishwa na Intaneti, kuweza kupata namna ya kutumia
Intaneti, na kujipatia huduma mbali mbali muhimi k.v. tovutu ya Shule
Direct na nyinginezo nyingi zipatikanazo kupitia Intaneti.
Mpango huu wa Internet.org unapatikana kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo kwa sasa.
www.shuledirect.co.tz Jifunze. Jadiliana. Wakati wowote. Mahali Popote.