Mtaalamu wa masuala ya usalama kwenye Mtandao Yusuph Kileo akiwasilisha mada |
Itakumbukwa katika mkutano uliofanyika mapema mwezi huu jijini "CAIRO" hofu
ya ukuwaji wa uhalifu mtandao unaoweza kurudisha nyuma uchumi wa
mataifa ya Afrika ulipata kujadiliwa kwa kina huku nchi ya Misri
ikionyesha washiriki wa mkutano huo jitihada inayoendelea nayo katika
kukabiliana na uhalifu mtandao.
Imeripotiwa na Mtandao wa "MGAFRICA" kuhusiana
na kilichojiri katika mkutano uliokamilika jijini Johannesburg, Afrika
kusini wa maswala ya usalama mitandao ambapo Bara la Afrika limetabiriwa
kuwa na ukuaji wa uhalifu mtandao kutokana na mikakati dhaifu ya
kujiweka salama huku ikiwapatia wahalifu mtandao urahisi mkubwa wa
kuleta maafa siku za usoni.
Kumeendelea
kuwa na wimbi kubwa la uhalifu mitandao ingawa jitihada za kukabiliana
na uhalifu huo zimeendelea kugharimu mataifa mengi hivi sasa. Mataifa
yamekua yakiwekeza kwenye maswala ya usalama mitandao lakini bado
wahalifu mtandao wameonekana kuendelea kutamba.
Mkutano
huo wa maswala ya usalama mitandao uliangazia kwa karibu sababu za
ukuaji wa uhalifu mtandao na nini kifanyike kwa mataifa ili kuweza
kupiga hatua ya kubaki salama kimtandao. Wataalam wa maswala Mtandao
kutoka katika mataifa mbali mbali walikutana kuyajadili mambo hayo yafuatayo:-
Swala
la kukuza uwelewa kwa watumiaji mtandao kuhusu matumizi salama ya
mitandao lilionekana bado ni changamoto katika mataifa mengi. Na njia
rafiki za kuhakiki kampeni hii ya kuhamasisha umma juu ya matumizi salama
ilipelekea mambo mengi kuangaziwa macho huku "TOVUTI" maalum kwa ajili ya uelewa wa matumizi salama mitandao ikipata kuzinduliwa.
Sheria
nazo zilionekana kuwa changamoto kubwa sana barani Afrika. Kumekua na
kusua sua sana kwa sheria mitandao kuanza kufanyiwa kazi huku Wataalam
kutoka katika vyombo vya sheria (Mahakama) wakionyesha hali
wanayokumbana nayo katika kutolea maamuzi dhidi ya uhalifu mtandao.
Tulipata
kufafanua na kueleza usalama mitandao haunabudi kwenda sambamba na
sheria zake maalum zinazopaswa kupitiwa mara kwa mara na kuborehwa ili
kuendana na wakati. Bila kufanya hivyo hali ya wahalifu mtandao kufanya
matukio na kutopatiwa adhabu stahiki itaendelea kuchangia ukuaji wa
uhalifu huu.
Swala
la Uhaba wa wataalam nalo halikubaki nyuma. Mjadala mkubwa uliangazia
jitihada mbali mbali za mataifa zinazofanywa ili kuweza kuwa na wataalam
wakutosha wenye uwezo sahihi wa kujua namna ya kudhibiti, kukabiliana
na kuzuia uhalifu mtandao.
Ushirikiano
katika maswala ya usalama mitandao kuanzia ngazi ya kitaifa kibara na
kimataifa ilionekana bado ni changamoto kubwa sana ambayo bado ku safari
ndefu kuhakiki tunafikia malengo. Njia rafiki ya kuhakiki tunakua na
utamaduni wa kushirikiana kuanzia ngazi ya taifa moja moja kabla ya
kuvuka mipaka ilisisitizwa kufanyiwa kazi ili kurahisisha vita dhidi ya
uhalifu mtandao.
Wataalam
mbali mbali walipata fursa ya kuonyesha kwa vitendo gunduzi mpya za
kisasa zenye kurahisisha uwezo wa kubaini, kuzuia na kukabiliana na
uhalifu mtandao ambapo kila gunduzi ilipata kujadiliwa kwa kina ili
kuweza kuleta tija dhidi ya mapambano na uhalifu mtandao.
Mataifa
na vikundi mbali mbali pia vilipata fursa ya kuonyesha takwimu mbali
mbali za maswala ya uhalifu mtandao na njia mbazo mataifa hayo
yameendelea kukabiliana na wimbi kubwa la wahalifu mtandao. Mjadala
mkubwa katika kuzikosoa na kurekebisha jitihada hizo ulipata kuonekana
wenye malengo madhubuti ya kuwa na bara salama kimtandao.
Paliangaziwa pia vifaa mbali mbali vya kiusalama mitandao ambapo
vimeendelea kutumika ipasavyo kuhakiki uhalifu mtandao unakabiliwa
ipasavyo. Huku pakitolewa baadhi ya vifaa hivyo kwa washiriki ili kuweza
kuongeza tija kwenye mapambano dhidi ya uhalifu mtandao katika mataifa
mbalimbali barani Afrika.
Na Yusuph Kileo