|
Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Prof Makame Mbarawa akihutubia |
|
Balozi wa China nchini Tanzania nchini Lu Youqing |
|
MC wa tukio Isaac Mruma toka TCRA |
|
Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania Prof Patrick Makungu na Mkurugenzi Mtenda wa HUAWEI Zhang Yongquan wakitia saini mkataba |
|
Mkurugenzi Mtenda wa HUAWEI Zhang Yongquan akihutubia |
|
Mitambo ya Data ya HUAWEI iliyotolewa |
|
Kituo cha Utunzaji wa Data kitakachojengwa Kijitonyama,jijini Dar es salaam kitakavyonekana baada ya kukamilika |
Jumla ya dola milioni 93.77 za
kimarekani sawa na takribani shilingi trioni 1.9 za kitanzania zitatumika kujenga mitambo ya
kituo cha kuhifadhia data cha Tanzania ikiwa ni mkakati wa serikali ya nchi hiyo katika
kujenga miundo mbinu ya teknolojia ya habari na mawasilino (teknohama) nchini.
Ujenzi wa mitambo hiyo umetiwa saini
kwenye mkataba baina ya Serikali ya
Tanzania na Kampuni ya mawasiliano ya HUAWEI leo jijini Dar es salaam ambapo
ulishuhudiwa na waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania,Profesa Makame
Mbarawa,Balozi wa China nchini Lu Youqing na wadau mbalimbali wa teknolojia ya
habari na mawasiliano toka serikalini na makampuni mbalimbali.
Waziri Makame Mbarawa amesema kuwa kituo hicho kitakachojengwa katika eneo
la kijitonyama jijini Dar es salaam kitakuwa ni kituo kikubwa katika ukanda wa
Afrika Mashariki na kati ikiwa ni hatua ya tatu baada ya ujenzi wa mkongo wa
Taifa na kitakuwa kikitunza data za Serikali,Makampuni ya simu na makampuni mengine binafsi.
Waziri Mbarawa amesema serikali inapaswa kuwekeza katika
teknolojia za kisasa ili kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali nchini Tanzania.