Friday, July 3, 2015

TTCL YAJA NA HUDUMA YA INTANET YA SATELAITI


Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), imeendelea kukuza matumizi ya mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEKNOHAMA) nchini Tanzania  ambapo kupitia kipindi cha msimu wa Sabasaba imeleta teknolojia ambayo itasaidia kampuni, taasisi na ofisi za Serikali ambazo ziko mbali na njia ya Mkongo wa Taifa kupatiwa mawasiliano ya intaneti kwa njia ya satelaiti.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo  jijini Dar es Salaam  kwenye Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa, katika viwanja vya Sabasaba, Ofisa kutoka TTCL, Fredrick Benard amesema teknolojia hiyo ni muhimu kwa kampuni na kwamba ina ubora, uhakika na kwa bei nafuu.

Benald amesema ili kupata huduma ya intaneti kwa njia ya setelaiti, mteja atapaswa kupeleka maombi rasmi ya huduma anayoitaka na baadaye atapelekewa tathmini ya gharama ya kuunganishiwa.

Aidha amesema, kampuni iliamua kupeleka huduma hiyo kutokana na mahitaji makubwa ya matumizi ya intaneti kwa shughuli za maendeleo.

Popular Posts

Labels