Moja
ya udhaifu mkubwa unaokumba mataifa mengi hasa barani Afrika ni
kutokua na mikakati ya uzuizi endelevu dhidi ya uhalifu mtandao.
Imethibitika kuwa nchi nyingi zimekua zikingoja tatizo litokee ndio
jitihada zinachukuliwa kutatua tatizo huku athari ikiwa imeshaonekana.
Mwaka
huu baada ya Nchi ya Ghana kuwa miongoni mwa waathirika wa uhalifu
mtandao ambapo mtandao mkuu wa serikali ya nchi hiyo inao hudumia
tovuti 58 za serikali ulidukuliwa na kusababisha tovuti 11 kuingiliwa na
kuathiriwa na wahalifu mtandao; Waziri wa mawasiliano wanchi hiyo Dr.
Edward Omane Boamah ametangaza mapambano dhidi ya uhalifu mtandao ili
kulinda usalama mtandao wa nchi hiyo.
Tukio
hilo la udukuzi baadae CERT ya nchi hiyo yenye dhamana ya kutambua na
kuzuia uhalifu mtandao kabla haujatokea pamoja na na kuhakiki usalama
mtandao wanchi hiyo unaendelea kubeba sura njema ilisema wahalifu
mtandao walifanikiwa kudukua tovuti hizo za serikali na kuziathiri
vibaya kutokana na mapungufu ya kutokua na program zinazoendana na
wakati katika tuvuti hizo.
Katika
hotuba iliyosomwa na Patricia Dovi Sampson kwa niaba ya waziri wa
mawasiliano wa Nchi hiyo katika jukwaa la wadau wa maswala ya usalama
mitandao Julai Mosi mwaka huu 2015, iliainisha kua nchi hiyo tayari
imetengeneza sera na mkakati wa taifa wa usalama mtandao (National Cyber
Security Policy and Strategy (NCSPS) document) ili kupambana na uhalifu
mtandao nchini humo.
Ikisisitiza
Hotuba hiyo ilieleza, Nchi hiyo inatambua kuwa uhalifu mtandao hauna
mipaka kwani wahalifu udukuzi wa tovuti za serikali ya nchi hiyo
ulionekana wametokea nchini Uturuki. Hivyo ikaelezwa, Nchi hiyo
itaimarisha zaidi ufanyaji kazi dhidi ya uhalifu mtandao kwa ushirikiano
na mataifa mengine ili kufikia malengo.
Hotuba
hiyo pia ilihimiza vyombo vya habari kuongeza jitihada za kukuza uelewa
wa maswala ya usalama mitandao kwa wanachi wa Nchi hiyo kwani uelewa
bado umekua mdogo sana unaosababisha uhalifu mtandao kuzidi kushika kasi
nchini humo na kuathiri uchumi kutokana na makampuni ya Kifedha ya Nchi
hiyo kuonekana kuathiriwa zaidi.
Aidha,
Mshauri mkuu wan chi hiyo katika maswala ya usalama Mtandao Bwana.
Albert Atwi-Boasiako, alieleza mafunzo ya uelewa yanayo paswa kufanywa
kwa taasisi za serikali na zisizo za serikali bado ya kiwango cha chini
sana kwa kiasi kikubwa hali inayo sababisha taasisi hizo kushindwa kuwa
na mikakati stahiki na endelevu ya kutambua na kudhibiti uhalifu mtandao
kabla haujatokea.
Hivyo
mshauri huyo alitoa Wito kwa taasisi hizo kua na mipango madhubuti ya
kujipatia elimu za ufahamu dhidi ya uhalifu mtandao ili kuweza kubaki
salama na kupunguza uhalifu mtandao unao kua kwa kasi Duniani kote.
Katika
kuhitimisha hotuba ya Waziri wa Mawasiliano Wa Nchi ya Ghana, wito
ulitolewa wa kua na njia rafiki ya ukusanyaji wa taarifa na kupata
Takwimu sahihi zitakazo onyesha kiwango cha uhalifu mtandao huku
intelijensia ya utokeaji wa uhalifu huo ikifanyiwa kazi ipasavyo ili
kuhimili vishindo vya uhalifu mtandao nchini humo.
Nini Taifa la TANZANIA linajifunza kutokana na hili?:
Ikumbukwe Tanzania pia imekua ni miongoni mwa nchi zilizo ainishwa kua
na tabia ya kukabiliana na uhalifu mtandao baada ya kutokea imeaminika
njia za kutambua na kudhibiti uhalifu kabla haujatokea bado ni tatizo na
jitihada za dhati zina hitajika.
Kwa
upande wa Sera na mikakati wa maswala ya usalama mitandao bado taifa
Halina kabisa hadi sasa kitu ambacho ni changangamoto kubwa katika
kupambana na uhalifu huu mtandao.
Pia
Uelewa na nguvu kazi watu imeendelea kua changamoto huku nguvu kazi
chache zilizoko kutotumiwa vizuri na taifa. Aidha, ushirikiano kuanzia
ngazi ya taifa pamoja na kuvuka mipaka bado umeendelea kua changamoto
kubwa inayo paswa kutafutiwa suluhu.
Upambanaji
na uhalifu mtandao lazima uwe na mikakati na kuhaki njia stahiki
zilizopendekezwa na wataalam wa usalama mtandao duniani kote zinafatwa
ipasavyo ili kuhakiki taifa linabaki salama kimtandao – Bado kumekua na
kusua sua kwa kuwekeza katika maswala ya usalama mitandao Nchini huku
Taifa kuonekana kupiga hatua kubwa katika maswala ya TEKINOHAMA ambapo
Serikali ya Awamu ya Nne imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwekeza katika
Miundo mbinu na ukuzaji wa matumizi ya TEKINOHAMA Nchini.
Ukuaji
huu wa kasi wa Miundombinu na utumiaji wa TEKINOHAMA ikumbukwe inaambatana
kabisa na ukuaji wa kasi wa uhalifu mtandao Nchini. Hivyo jitihada za
dhati na haraka katika kukabilia na Hali tete ya hapo baadae kimttandao
zina hitajika hasa Baada ya TANZANIA kuorodheshwa kua ni Nchi ya 6
Inayotegemewa kuathirika zaidi na uhalifu mtandaokatika mwaka wa
2015/2016 huku Ransomeware kwa mara ya kwanza kuonekana kuathiri taifa
la Tanzania.