Kundi
jipya lenye makao yake barani ulaya linalounganisha pamoja nchi wanachama wa
bara ulaya pamoja na Canada, Colombia, Australia na marekani limedhamiria
kuunganisha mataifa mengine na kuhakiki maswala mbali mbali yahusuyo usalama
mtandao yanafanyiwa kazi ipasavyo.
Katika
andiko la naibu mkurugenzi wa chombo cha uingereza kinacho shughulikia maswala
ya uhalifu mtandao pamoja na kiongozi wa
kundi jipya la muunganiko wa nchi la kukabiliana na uhalifu mtandao wame elezea ukuaji wa changamoto mbali mbali kwa vyombo vya
usalama katika mataifa mengi na kusisitiza kuna umuhimu mkubwa wa kuunganisha
nguvu za pamoja ili kuweza kufanikiwa katika vita dhidi ya uhalifu mtandao.
Chombo cha upelelezi cha Marekani (FBI) kimebainisha kulipa kipaumbele cha juu swala la mapambano dhidi ya uhalifu
mtandao kutokana na kilicho zungumzwa na mkurugenzi wake ya kuwa nchi hiyo
tayari imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupambana na wahalifu wanao onekana na kwa
sasa wahalifu mtandao kua ndio changamoto yake kubwa na hivyo wameazimia kuanza
mapambano na uhalifu huo.
Kwa
upande mwingine katika mkutano mkuu wa maswala ya usalama mtandao wa mwisho wa
mwaka ambapo nimeteuliwa kuwa katika panel ya washauri mada zinazotegemewa
kujadiliwa na wataalam kutoka maeneo yote duniani ni pamoja na kutafuta njia
rafiki ya kufikiwa kwa malengo ya kuunganisha hasa bara la afrika kuweza kuwa
na njia ya pamoja ya kupambana na uhalifu mtandao huku maswala ya kisheria za kimtandao yanavyo sumbua mataifa mbali
mbali nini utatuzi wake.
Na:Yusuph Kileo