Picha kwa hisani yan http://www.sligotoday.ie |
Jeshi
la Polisi kikosi cha usalama Barabarani nchini Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya
usafiri wa Nchi kavu na Majini SUMATRA limeanzisha mkakati wa kuwafungia
leseni madereva watakaobanika kuendesha magari huku wakiwa manazungumza
na simu za mkononi.
Zoezi
hilo limekuja kufuatia kile kinachodaiwa kuwepo kwa ongezeko la ajali
za barabarani ambazo zinasababishwa na uzembe ambao unasababishwa na
unywaji wa pombe,kuchoka na kuzungumza na simu hizo.
Takwimu
zinaonyesha kuwa kumekuwa na ongezeko la matukio 264 ya ajali
barabarani kwa mwaka 2013 sawa na asilimia 1.1 tofauti na mwaka 2012
ambapo matukio yalikuwa 23,578.
Kwa
mwaka huu kati ya januari hadi June idadi ya ajali zilizoripotiwa
zilikiwa 8,405 zilizosababisha vifo 1743 na majeruhi 7,523 hali ambayo
Kamanda Mpinga anasema ipo mikakati mbadala ya kukabiliana na hali hiyo.
Inatajwa
kuwa madereva wengi hawana tabia ya kupima afya zao mara kwa
mara,inaelezwa kuwa magonjwa ya macho,kisukari pamoja na shinikizo la
damu pia linachangia ajali nyingi.