Kikundi cha kihalifu mtandao cha #Anonymous kimetekeleza mashambulizi mtandao dhidi ya Nchi ya Angola na kufanikiwa kudukua na kuangusha Tovuti 20 za serikali ya Nchi Hiyo.
Hatua hiyo ya kikundi hicho imefuatia baada ya kushinikiza serikali ya Nchi hiyo kuwaachia watu 17 waliokamatwa kutokana na uasi dhidi ya Serikali ya Rais Jose Eduardo dos Santo.
Tukio hilo la Mashambulizi limepokelewa kwa masikitikomakubwa na jumuia ya wana usalama mitandao huku usaidizi wa dhati kuimarisha usalama kwa tovuti za Nchi hiyo zikichukuliwa.
Matukio ya kushambulia Serikali za Nchi za Afrika kimtandao yamepata kuonekana mara kadhaa ambapo Ghana pia ilipata kua muathirika.