Watu wengi
wameshaona filamu ambazo wahalifu
wakidukua simu za mikononi hata kama zimezimwa.
Kama
ilivyozoeleka kuwa watu wengi hufikiri mambo hayo ni ya kufikirika.
Hata hivyo
hivi karibuni kampuni ya AVG inayojihusisha na masuala ya usalama katika simu
za mikononi na imegundua virusi aina ya malware kilichopewa jina la ‘PowerOffHijack,’ambavyo vinauwezo
wa kuingilia mfumo wa kuzima simu na kuifanya simu ya mkononi iendelee
kupatikana japo imezimwa..
Kirusi huyo
mara ya kwanza ameonekana nchini China na kusambaa katika program tumishi za uchina
na simu nyingi zimeshambuliwa na kirusi huyo hasa zilizotengenezwa kwa program
endeshi za Android zenye zaidi ya toleo namba 5
Kirusi hicho
kikiingia kwa simu ya mkononi simu itatoa ujumbe kuwa imezimwa na malware itawe
kupiga simu,kupiga picha na kufanya mambo mbalimbali bila mwenye simu kutambua.