Mamlaka ya
Mawasiliano nchini (TCRA) na Shirika la umoja wa mataifa la Mawasiliano ya simu
ulimwenguni ITU kwa pamoja wameridhia
makubaliano ya kusitisha Mfumo wa utangazaji wa televisheni unaotumia teknolojia ya analojia katika miundombinu
ya minara ifikapo juni 17,2015 na kuanza kutumia mfumo wa utangazaji wa
kidijitali pekee.
Akizungumza
na waandishi wa habari hii leo jijini
Dar es salaam Meneja mawasiliano wa TCRA Innocent
Mungy amesema makubaliano hayo ya jumuiya za ushirikiano
wanchi mbalimbali zimechukua hatua za pamoja kuhakikisha uhamaji kutoka mfumo
wa utangazaji wa anolojia kwenda dijitali unafanikiwa.
Mungy
amesema Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kutekeleza maazimio ya nchi wanachama
na uzimaji wa mitambo ya televisheni inayotumia teknolojia ya analojia Tanzania Bara
ilianza kufanyika desemba 31,2012 .