Wataalamu wa Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Pennsylvania
na Chuo Kikuu cha Vijana cha Bringman nchini Marekani wamebaini kuwa matumizi
ya simu ni chanzo cha kutofurahia maisha na kuongeza msongo.
Utafiti uliofanywa na wataalamu hao chini ya usimamizi wa
Brandon McDaniel,Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Pennsylvania,ulibainisha kuwa
watu wengi wanaongeza umaskini wa kujitakia kwa kutumia muda mwingi kwenye
simu.
Wanazungumzia maisha ya watu,mafanikio yao,kushindwa kwao
badala ya kuangalia vitu vitakavyowaingia fedha zaidi,inaeleza sehemu ya
utafiti huo.
Utafiti huo ulibainisha kuwa mbali na umaskini wa
kujitakia,matumizi ya simu kupita kiasi huchangia kwa asilimia 75 ndoa
kuvunjika pia hatari ya kupata msongo wa mawazo.
Utafiti huo uliohusisha watu wazima 867 wenye umri wa miaka
30 hadi 45,ulibainisha kuwa kama wasingekuwa na simu,robo tatu ya watu hao
wangekuwa wamefanya mambo mengi kuboresha maisha yao ikiwemo utendaji bora wa
kazi.
Majibu ya utafiti huo yalionesha kuwa wanandoa wengi
wangepata muda wa kujadili namna ya kumaliza tofauti zao,kufikia
mafaniki,kutimiza malengo hata kuboresha penzi kama wasingetumia simu.
Takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA)
zinaonesha kuwa mwaka 2014 kulikuwa na laini za simu za mkononi zipatazo
31,862,656,ikilinganishwa na laini 2,963,737 mwaka 2005,watumiaji wa intaneti
wameongezeka hadi kufikia 11,000,000 Desemba mwaka 2014 kutoka 3,563
waliokuwepo mwaka 2008
Chanzo:Gazeti la Mwananchi