Ni uchukuaji wa taarifa za mwingine kwa njia ambazo sio
halali kwa kutumia vyombo vya mawasiliano anavyotumia mtu husika kama email ,
simu , kompyuta , tv na vingine vingi .
Taarifa hizi zinaweza kuwa kwa njia ya nyaraka
zilizohifadhiwa , zinazofanyiwa kazi ( kama ziko shared ) , kusikiliza
mawasiliano ya sauti kama kupiga au kupokea simu , ujumbe mfupi yaani sms na
Mawasiliano ya email mtu anayofanya na watu wake au makundi .
Katika siku za karibuni wigo umepanuka kidogo sasa hivi mpaka
kwenye anuani za watu kwenye mitandao ya kijamii kama facebook watu wanaouwezo
wa kuiba taarifa au kuingia na kupotosha , kwenye majukwaa ya majadiliano pia
watu wanaweza kuingia kuvuruga au kuiba taarifa za mtumiaji fulani bila wenye
jukwaa kujua .
Kwa mataifa yaliyoendelea Aina hii ya Ujasusi ni njia moja
wapo ya kujilinda dhidi ya adui wa nje na wa ndani , adui huyo anaweza kuwa
gaidi , jasusi mwenzake , biashara za kimataifa , teknolojia , uuzaji na
usambazi wa silaha , taarifa za afya , viwanda na nyingine nyingi .
MATUKIO MAARUFU YA UDUKUZI KIMATAIFA
1 – Miezi kadhaa iliyopita tumesikia na kusoma kwenye vyombo
vya habari kuhusu Udukuzi uliokuwa unafanywa dhidi ya viongozi mbalimbali wa
nchi za ulaya na amerika ya kusini na mashirika ya ujasusi ya kimarekani .
2 – siku kadhaa kabla ya mkutano wa G20 NA hata wakati
mkutano huo unaendelea baadhi ya wajumbe walipokea barua pepe ambazo zilikuwa
na program maalumu zilizojiingiza kwenye kompyuta zao na hapo hapo walianza
kufuatiliwa na kuibiwa taarifa zao haswa kile walichokuwa wanafanya na kuandika
kutumia kompyuta zao na simu , uchunguzi ulipofanyika iligundulika uvamizi huu
ulitokea uchina .
3 – wajumbe wa mpango wa nyuklia wa irani walipoenda
uingereza kwa ajili ya mkutano Fulani nao waliingiziwa virusi walipowasha tu
vifaa vyao vya mawasiliano , virusi hivi vilisambaa mpaka kwao mpaka kwenye
vinu vyao vya nyuklia matokeo yake ni kwa baadhi ya vitu kutokufanya kazi
sawasawa .
Hili suala kwa Irani pamoja na vikwazo ndio limesababisha
uongozi mpya kutaka muafaka na mataifa yaliyoendelea , pia lilisababisha baadhi
ya wanasayansi wao kuuwawa kwa njia za kigaidi haswa wale waliokuwepo kwenye
mradi huu .
MATUKIO MAARUFU YA UDUKUZI NCHINI
Kwa hapa nchini kuna matukio 3 ambayo ni maarufu lakini
hayajawahi kuongelewa sana .
1 – Waziri mmoja na kundi lake walikuwa wanaenda nchi Fulani
ya ulaya kwa ajili ya warsha na alitarajiwa kutoa msimamo Fulani , basi
alivyofika hotelini kuwasha kompyuta yake kuanza kupekua vitu hapo maharamia wa
mtandao walimvamia na kuharibu hiyo kitu aliyokuwa anafanyia kazi siku zote .
2 – Mara kadhaa kumewahi kutokea udukuzi kwenye taasisi zetu
zinazosimamia maswala ya mawasiliano haswa TCRA na ilipochunguzwa ikagundulika
waingiliaji wengi walitokea nchi ya China , china imekuwa nchi inayongaa
ulimwenguni kwenye masuala ya Udukuzi .
3 – Udukuzi uliwahi kufanywa dhidi ya shirika moja la ndege
nchini halafu wahalifu wakavamia kwa nia ya kuharibu utaratibu wa urushaji
ndege na uhifadhi mwingine wa taarifa , hii ilisababisha ndege moja kukaa
uwanjani bila kufanya safari kwa mwezi mmoja kwa sababu za kiusalama na ndege
hiyo ilikuwa inaendeshwa na mitambo maalumu kutoka nchi nyingine .
HALI YA TANZANIA
Hali ya Tanzania kusema za ukweli sio ya kuridhisha sana
kutokana na mambo 3 makuu .
1 – Sheria za Mawasiliano – Sheria zetu za mawasiliano
hazijitoshelezi na wahalifu wengi wanatumia fursa hiyo kufanya uhalifu wao
kutoka hapa kupiga wengine au kupitia hapa kupiga wengine wa mbali , tunapenda
kuwa na sheria nzuri za mawasiliano zinazoendana na wakati wa sasa na kila
idara serikalini itengeneze sheria zake kwa kunukuu sheria mama .
2 – Utumiaji wa Vifaa chakavu – Tunaona watu haswa wenye
fedha zao wakinunua vifaa chakavu vya mawasiliano haswa toka nchi za mbali kwa
ajili ya kuja kutumia hapa nchini vifaa hivi vingi vimesababisha utengenezwaji
wa njia za kivamizi na kwa sababu teknologia zake za kizamani imekuwa rahisi wa
wahalifu kuzichezea na kufanya wanachojua .
3 – Vifaa visivyokidhi viwango – Tumeona watu wananunua simu
ambazo hazina viwango na kuzitumia kwenye shuguli za uhalifu , simu nyingine
zinapunguzwa baadhi ya vitu ili ziweze kufanya kazi nchini , watu maofisini
wanaingiza programu kwenye kompyuta zao ambazo hazina leseni au leseni bandia yote
hii haitakiwi .
4 – Kutokufuata taratibu za manunuzi – Hapo juu nimesema
hatuna sheria za mawsiliano na tumezoea kununua vifaa chakavu , tukiwa na hivyo
viwili tutaweza kuwa na utaratibu mzuri wa kununua vifaa haswa vya mawasiliano
maofisini na kwenye idara za serikali utakaofuata vitu hivyo viwili .
NINI KIFANYIKE
Ni wakati mzuri sasa kwa Taasisi muhimu nchini kama Mabenki ,
Polisi , Tume ya mawasiliano , Kampuni za Mawasiliano ya Simu na Intaneti ,
taasisi za elimu kama vyuo na shule kuwa na taratibu za kufundisha watu
matumizi salama ya vifaa vya mawasiliano , ununuzi mzuri wa vifaa vya
mawasiliano na uuzaji mzuri wa vifaa vya mawasiliano .
Tufanye hivi huku tukingoja sheria mama wa mawasiliano
iboreshwe na wengi wataboresha masomo yao kuzingatia sheria mama ya mawasiliano
nchini kulingana na hali tuliyonayo .
Ningependa kuona sheria mama ikiandikwa kutokana na mila na
tamaduni za mtanzania sio nje ya hapo , hata pale mtu akisoma itoe harufu ya
utanzania au uafrika mashariki .
Kupambana na udukuzi wote sio rahisi lakini tunaweza
kupunguza uwezo wa kufanyiwa udukuzi kwa kuhakikisha tuna vifaa vizuri vya
mawasiliano na kufuata taratibu za utumiaji .
YONA FARES MARO
0786 806028