Virusi wa malware waliwekwa kwenye ATM kwa kutumia flash za USB |
Mwishoni mwa mwaka 2013 watafiti wamegundua namna wahalifu kwa njia ya mtandao walivyotumia mbinu ya
virusi vya komputa waitwao malware na
kuzifanya pesa zitoke zenyewe katika mashine za ATM.
Taarifa ya watafiti hao iliyotolewa katika kongamano la wataalamu
wa mifumo ya komputa lililofanyika Disemba
28,2013 huko Hamburg,Ujerumani inaonesha
kuwa wezi hao walifanya wizi huo katika banki ambazo hazikutajwa majina katika
nchi za Ulaya mwanzoni mwa mwaka 2013 ambapo walikuwa wakitoboa matundu na
kuweka flash USB zenye namba maalum( code) katika mashine hizo za banki za kutolea
pesa.
Watafiti wawili ambao wamegundua mbinu zilizotumika
kufanikisha uhalifu huo ambao wameomba kutotajwa majina yao wameeleza kuwa
uhalifu huo unaonesha kuwa wezi hao hawakuwa wakiaminiana .
ATM hizo zilikuwa zikitumia Windows XP. Ambapo wamiliki wa banki
waligundua kuwa wahalifu walikuwa wakituma virusi kwenye komputa na kuiharibu
mifumo ya faragha na kusababisha kuingia katika komputa za benki mara kwa mara
bila kugundulika.
Shirika la Utangazaji la BBC limeeleza kuwa wahalifu hao
walikuwa walitumia namba maalum zenye tarakimu 12 ambazo ziliruhusu kiwango cha
pesa kiweze kutoka kupitia ATM na taarifa za kibenki kurudi katika komputa
ambapo ATM ilitoa mwongozo wa kile kilichotakiwa na wahalifu.
Watafiti wamesema
iwapo namba hizo hazikuwa zimeingizwa mara tatu, mashine ilirudi katika
mwongozo wake wa kawaida hii inaonesha
kuwa kulikuwa na kutoaminiana miongoni mwa wahalifu hao.