Rais Barrack Obama aalitarajiwa juma lilopita kutangaza ambavyo angeweza kurudisha
imani katika idara ya ujasusi nchini Marekani kufuatia kufichuliwa kwa taarifa za
idara hiyo na aliyekuwa mchambuzi wa maswala ya kijasusi nchini humo Edward
Snowden.
Ufichuzi wa hivi karibuni uliochapishwa siku ya alhamisi
unadai kuwa idara hiyo ya ujasusi ilidukua mamilioni ya ujumbe katika simu za
watu za mkononi duniani kila siku.
Upelelezi huo wa simu zilizopigwa pamoja na mitandao umezua
hisia kali kutoka kwa wanaharakati na makundi ya kijamii nchini marekani na
washirika wake.
Hata hivyo vitengo vya ujasusi vimeonya kuwa uchunguzi zaidi
wa mienendo yake huenda ukaathiri usalama wa marekani.
Chanzo:bbc