Hebu jibu haraka-haraka! Ulikuwa wapi Jumanne iliyopita
majira ya saa 12:35 jioni? jibu lako huenda likawa hivi “Mimi… sina kumbukumbu
iwayo yoyote ile.
Kwa kweli akili za watu wengi hazitendi kazi kwa mfumo huo.
Lakini uwezekano mkubwa ni kwamba, Google wanafahamu ulipokuwa. Bila shaka
wanafahamu mahali ulipokuwa siku nyingine nyingi, vilevile. Nao wanao uwezo kabisa
kukufahamisha, wakikuruhusu kuyaishi mapito yako upya hatua moja baada ya
nyingine.
Kama unatembea na kifaa chochote kiendeshwacho na Google
(kama vile simu aina ya Android au tabiti (tablet)), basi kulikuwa na swali
wakati wa kukiunganisha kifaa hicho endapo ungependa Google itoe taarifa kwa
mitambo yake mikuu kwamba upo mahali gani. Hii ndiyo habari.
Unajua ni kwa jinsi gani Google sasa inao uwezo wa
kimazingaombwe wa kufahamu ni wapi ufanyapo kazi na kukutahadharisha juu ya
misongamano ya magari katika barabara unayoitumia? Hiyo taarifa uliyoiruhusu
mwanzoni wakati ukiunganisha kifaa chako ndiyo inayowezesha jambo hili.
.Anglizo : kama umekuwa ukifuatilia kwa makini, huenda
ulishaliona hili huko nyuma. Si jambo geni. Kwa kweli, limekuwepo kwa miaka
kadhaa. Hata hivyo, Greg Kumparak anaeleza kuwa ilikuwa wakati murua kabisa kubaini watu wengi tu
ambao walilifahamu hili, hata alipowahoji marafiki zake ambao wao wamekaa
kiteknolojia zaidi. Hivyo basi, chukulia hili kama tangazo lenye kustusha kwa
manufaa ya umma.
Kwa kweli ni jambo la kushtua, katika viwango vyake;
linawafanya watu kufikiria ni kiwango
kikubwa kiasi gani cha habari wanazozikusanya Google. Lakini habari yoyote
iliyopo pale, iko pale kwa sababu wewe uliwapa dole gumba la ndiyo wakati
fulani, hata kama ilikuwa ni kwa kutokutafakari, wewe ukabonyeza vitu fulani
wakati unakiunganisha kifaa chako kipya.
Endapo kwa ghafla sasa unaanza kutambua kwamba kuna mahali
fulani hivi ulikuwa unapatembelea ambako usingependa pawepo katika historia
yako (mimi simhukumu mtu hapa jamani), basi unaweza ukafuta kumbukumbu hiyo
siku-kwa-siku ama kuifuta kumbukumbu yako yote ya wapi ulikuwa kwa ujumla wake
kwa mkumbo mmoja.
Google walizindua mfumo wa kwanza wa kifaa hiki kipindi kile
kile walipoanzisha programu tumishi ya Latitude. Baada ya kuondoa Latitude, waliiacha
kivinjari chake, wakiinakshi na kuiongezea umaridadi fulani-fulani kadri muda
ulivyosonga. Mbinu mojawapo iliyo poa sana: pitisha kielekezaji (mouse) chako
chini ya grafu (jedwali) pale chini yake. Ramani itakayojitokeza juu yake
itaonyesha mapito yako ya siku nzima, kutoka mahali hapa ulipokuwa hadi mahali
pengine ulipokwenda.
Greg Kumparak anasema yeye alitumia saa moja hivi na ziada,
nakisha upya tena mwezi mmoja uliopita
wa maisha yake,akijaribu kukumbuka kila kituo kilikuwa kwa makusudi yapi. Oh,
na ile grafu (jedwali) Yenyewe inanakili umbali uliotembea ukishabihiana na
muda uliotumika kutoka pale ulipoianza siku yako (hivyo, kwa walio wengi, ni
kuanzia nyumbani kwako), yote hii ni pamoja na jumla ya umbali uliotembea kila
siku.
Chanzo:Techcrunch.com