Miaka michache iliyopita kulikuwa na changamoto ya kuhifadhi
vitu sehemu ambayo mtu anaweza kutumia akiwa popote duniani akiwa ameunganishwa
na mtandao kwa njia ya yoyote ile kama ni simu ya mkono au computer .
Siku hizi changamoto hiyo imekwisha kama sio kupotea kabisa
zimebaki changamoto nyingine zaidi zinahusiana na ulinzi na usalama na hizi
hifadhi na hata uwezo wa mawasiliano wa vifaa vinavyotumika na kampuni
zinazotoa huduma hizi .
Wengi wetu tunatumia huduma mbalimbali kwa njia ya mtandao
kama ya simu za mikono , computer na vifaa vingine bila kujiuliza taarifa zote
hizo zinazokusanywa zinahifadhiwa wapi je ni kampuni ya simu kama ni simu yako
ya mkono ?
Umewahi kujiuliza barua pepe zako , tovuti zako , zinahifadhiwa
wapi na kwanini unaweza kuangalia popote ulipo duniani ambapo hakuna masharti
Fulani Fulani kama uchina na baadhi ya nchi zenye sharia ?
Ukiwa nchi jirani ya Kenya na ukiwa mteja wa safaricom Kenya
, unaweza kupatiwa huduma ya kuhifadhi vitu vyako unavyotumia kwenye kompyuta
yako na simu yako hata pale vifaa hivyo vinapopotea taarifa zako utaweza
kuzipata wa sababu vitakuwa vimehifadhiwa .
Nchini Tanzania nimeona mabenki yakitumia huduma hizi na
baadhi ya kampuni kubwa lakini shida imekuwa ni katika mawasiliano na njia
wanazotumia kuhifadhi hizo taarifa zao kiasi kwamba umeme ukikatika pale
wanapohifadhi pale hakuna kitu .
Siku moja wa mawaziri mmoja wa Tanzania alikuwa na ziara ya kikazi
ulaya sasa akapoteza ipad yake , simu ya mkono na laptop ambayo kulikuwa
kimehifadhiwa baadhi ya nyaraka zake ilibidi kutumia mlolongo mrefu sana kuja
kupata hizo taarifa huku nyumbani .
Fikiria hiyo wizara ingekuwa inatumia huduma nzuri za cloud
za kuhifadhi taarifa zake ina maana angeweza kupata sehemu yenye mawasiliano tu
kama ubalozini au hotelini kwake akalogin kwenye system ya wizara yake na
akachukuwa taarifa aliyokuwa anataka au angeamua kununua simu nyingine ni kiasi
cha kuingiza jina yake na namba ya siri basi vitu vyote vinashuka.
Sasa tufungue macho kuhusu huduma za kuhifadhi vitu kwa njia
ya mtandao maana huduma za mawasiliano ni nyingine na vifaa vyake na hata
gharama zake zimeshuka sana , badala ya kufikiria kununua server kubwa ndani ya
ofisi yako ambayo huna uhakika wa kutoa taarifa unapokuwa nje ya nchi kwanini
usihamie kwenye mfumo wa cloud ?
Kuna kampuni za kitanzania zina miradi sehemu mbalimbali
nchini na nje ya nchi na zina wafanyakazi wanaosafiri kwenye site hizo kwa
ajili ya kazi mbalimbali , hawa wafanyakazi hawahitaji kubeba taarifa nyingi
kwenye kompyuta zao na nyeti kwa ajili ya kazi badala yake walitakiwa wawe
wanazipata toka kwenye huduma hizi popote wanapoenda .
Mfumo wa cloud wa kuhifadhi vitu kwa njia ya mtandao una faida , hasara na changamoto nyingi sana
, kwa upande wa faida inajulikana wazi kuhusu kuboresha kazi , ukaribu na
shuguli zako na gharama zake , kwa upande wa hasara na changamoto ntajadili
kidogo hapa chini .
……………………………………………………………………………… …..
Siku za karibuni kuna kumetokea malalamiko toka ujerumani
kuhusu kampuni za marekani kuchungulia au kuona taarifa zao zinazohifadhiwa kwa
mfumo huu na tujue tu kwamba kampuni kubwa na nyingi zinazotoa huduma hizi ni
za kimarekani .
Kwahiyo kuna uwezekano wa kuibiwa taarifa za siri au kuvuja
kwa vitu kutegemeana na kampuni unayotumia au watu wanaofanya shuguli hizo
wenye uwezo wa kulogin kwenye system .
Mfumo huu una husisha server zinazohifadhi taarifa sehemu
mbalimbali duniani na sheria za mtandao ( cyber law ) ni tofauti kati ya nchi
na nchi , baadhi ya nchi hamna kabisa kama ya kwetu hii inatoa mwanya kwa
baadhi ya makosa kutendeka .
Kampuni zinazotoa huduma hizi nazo hufanya backup kama
dharura yoyote itatokea , maana yake hata taarifa zako unazohifadhi nao
wanakuhifadhia sasa hatujui wewe ukifuta kama nao wanafuta .
ITAENDELEA SIKU NYINGINE
YONA F MARO