Na:Brown Nyanza
Kampuni ya
Google mapema juma lilopita katika tukio la kuzindua kifaa chake cha chromecast na tabiti yake mpya ya Nexus 7, Imetoa takwimu
ambazo zinaiweka Hifadhi yake ya program tumishi iitwayo “Google
play” kuwa ndio inayoongoza kwa kuwa na program tumishi nyingi duniani ikiiacha nyuma hifadhi nyingine ya progam tumishi inayomilikuwa na Apple iitwayo Apples Store.
“Google
play” Ina jumla ya program tumishi (applications) zaidi ya milioni moja, Wakati
Apple’s App store ina jumla ya program tumishi laki tisa. Programu tumishi hizo
ni pamoja na vitabu vya mtandao (digital books), muziki, michezo ya tarakirishi (games), vipindi vya televisheni
na mengineyo mengi.
Chanzo:(www. gsmarena.com)