Serikali ya Tanzania imesema sheria ya kupambana na uhalifu
kwenye mitandao iko kwenye mchakato.
Waziri wa Mawasiliano ,Sayansi na Teknolojia wa Tanzania
Profesa Makame Mbarawa amesema hivi karibuni jijini Dar es salaam kuwa sheria
hiyo itakuwa imekamilika ili kukupambana na uhalifu kwenye mitandao mbalimbali.
Akizungumza katika mkutano maalum wa kuangalia changamoto na
hatua mbalimbali za kimaendeleo katika sekta ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano kwa nchi zilizo katika ukanda wa Bonde la Ufa uliofanyika jijini
Dar es salaam,Waziri huyo amesema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imeanzisha kitengo maalum ambacho
kazi yake ni kupambana na uhalifu wa mitandao.
Amesema kama kutakuwa na uhalifu umetokea katika nchi jirani
basi wananchi watapewa taarifa ili wachukue tahadhari.
Naye Kamishna wa
miundo mbinu na Nishati kutoka Umoja wa Afrika (AU),Dk.Elham Mahmod Ibrahim aliyekuwa amehudhuria mkutano huo
aliwatahadharisha na kuwataka mawaziri wa ukanda wa bonde la Ufa waliohuduhuria
mkutano huo kuwa wakali katika kuhakikisha sheria zilizowekwa katika kupambana
na wahalifu wa mitandao zinafuatwa na kuchukua mkondo wake.