Na:Yona Maro
Katika siku za karibuni kumetokea wizi wa aina mbalimbali
unaohusisha alama za vidole au vidole vya mtu pale anapotumia vidole
hivyo kwenye shuguli mbalimbali haswa zinazohusiana na kuandika maneno
ya siri .
Ndugu msomaji unaweza kuwa huamini au unaweza
kushangaa tu lakini inawezekana mtu wako wa karibu aliyeibiwa kitu kwa
njia ya mtandao au njia nyingine kwanza aliibiwa alama za vidole
zikatumika kwenye shuguli hizo .
Kama wewe ni mtumiaji wa simu za mikono haswa na
umewahi kwa mfano kubadilisha touch screen yako , au umewahi kubadilisha
keyboard au hata kwenye computer yako umewahi kubadilisha vitu hivyo na
kutupa jalalani au kama ni maeneo ya mjini basi wafanya usafi
wamekusanya .
Hawa wafanya usafi huwa wanaenda kuuza vifaa hivi
kwa watu wengine wanaojifanya wananunua screper lakini target yao kubwa
inakuwa ni alama za vidole wanaweza kutumia baadhi ya vifaa kuweza
kuonyesha ni herufi zipi unazoandika mara kwa mara , jinsi unavyoandika
na alama haswa ya vidole vyako .
Kuhusu simu ni watu wengi wameuza simu zao kwa washkaji au kutoa
zawadi tu bila kujiuliza mwisho wa yote ni nini , kama ulikuwa unatumia
simu sana kwa ajili ya kuingia kwenye benki yako kwa njia ya mtandao au
kufanya manunuzi au kuhifadhi vitu kwa namba za siri , ujue vitu hivyo
vinaweza kurudishwa na vikatumika dhidi yako .
Kama uliwahi kutembelea baadhi ya benki huwa
wanapenda kuwaambia watu wasiegemee vioo au sehemu nyingine za kushika
shika na hata unapoandika ndani ya benki hakikisha hiyo karatasi haiachi
alama yako kama sahihi , alama za vidole unapokandamiza au chochote
kile .