Unaweza kufanya vitu vingi vya maana kwa kutumia simu yako
iliyotengenezwa kwa mfumo wa Android
mbali na kupiga,kupokea simu,huduma ya ujumbe mfupi wa simu na intaneti.
Mojawapo ya mambo ya kuvutia katika simu za Android ni
kuitumia kuwa na mfumo wa mlio wa kuzuia wezi,kama ilivyo katika simu za iphone
ambayo hutumia program tumishi ya Find My Iphone.
Kuna program tumishi nyingi ikiwemo ya Google iitwayo Android Discovery Manager ambayo
inafanya kazi kwa watumiaji wa simu walio na barua pepe za google ambayo
huwezesha kufahamu eneo ilipo simu yako.
Pia kuna program tumishi ambayo huwezesha simu yako kutoa
mlio iwapo mtu atahamisha simu yako mahali ilipo,nyingine ni ile inayopiga
picha kwa camera ya mbele kwa mtu atakayejaribu kufungua simu yako kwa
kuuingiza neno la siri la uongo.
Kuna program tumishi iitwayo Anti Theft Alarm inayopataika
katika Google Play Store ambao inazuia
simu yako ya Android katika aina
mbalimbali za wizi.Program hii tumishi ya kuzuia uhalifu na inaelezwa kuwa ni
miongoni mwa program tumishi bora za kuzuia wizi wa mitandao ambapo mtu anaweza
kutumia kuzuia wizi wa komputa mpakato,nyaraka,barua pepe n.k ambapo nayo
huwezesha simu kutoa mlio mtu anapoihamisha ilipowekwa.