Cristiano Ronaldo, akicheza wakati wa mechi kati ya Ureno na Ufaransa. |
Mchezaji nyota wa timu ya soka ya Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo,amefanikiwa kuwa mwanamichezo wa kwanza kuwa na mashabiki milioni 100 wanaomfuatilia kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.
Takwimu hizi zinamfanya Mchezaji huyo ambaye pia huichezea timu ya soka ya nchi yake ya Ureno kufikia kiwango cha zaidi ya takribani mashabiki milioni 30 kwenye mtandao huo ya wale wanaomfuatilia Mchezaji bora wa mpira wa miguu Duniani Lionel Messi toka Argentina ambaye huchezea timu ya FC Barcelona ya Hispania.
Takwimu hizi ambazo huenda zikamwongezea thamani ya kibiashara mchezaji huyo ikiwemo kupata matangazo ya makampuni mbalimbali ambaye pia ana mashabiki milioni 30.5 wanaomfuatilia kwenye mtandao wa kijamii wa twitter,kwanitukio la hivi karibuni ambapo Christian Ronaldo kwa siku mbili aliandika mapachiko sita kwa muda wa siku mbili akitangaza saa aina ya TagHeuer, tangazo ambalo lilitazamwa mara milioni 34.9 kwenye facebook na kupata likes milioni 2.4 kwenye mtandao huo na kuipatia kampuni ya kutengeneza saa hizo thamani ya paundi 300,000.
Christian Ronaldo katika tangazo la saa za Tag Heuer |
Mwanzoni mwa mwezi huu Mchezaji wa Manchester United Wayne Rooney alikuwa mchezaji wa Kwanza wa Ligi ya Uingereza -PLF kufikisha mashabiki milioni 10 wanaomfuatilia kwenye mtandao wa Twitter.