Idara ya
uwakili ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Duniani imesema kuwa Utoaji wa semina na makongamano kupitia mtandao wa intaneti unaweza kuwafikia watu wengi kwa gharama ndogo kuliko njia za kawaida zinazotumika sasa.
Hatua hiyo inakuja baada ya hivi karibuni kufanyika mkutano wa uwakili kwa njia ya
mtandao uliowezeshwa na idara ya mawasiliano ya
kanisa hilo duniani na kuwashirikisha watu 2000 toka nchi 83 uliohusisha masaa 12 ya
mafunzo yaliyowezeshwa na watoa mada 15
wakiwemo Mwenyekiti wa Kanisa hilo ulimwenguni Mch Teddy Wilson,Makamu wake Mchungaji
Pardon Mwansa, Benjamin Shoun ,Mwenyekiti wa Divisheni ya Amerika ya Kati Israel Leitona Daniel Jackson toka Divisheni ya
Kaskazini mwabara la Amerika.
Taarifa zinaeleza kuwa mkutano huo ulitumia dola za kimarekani
20,000 tofauti na utaratibu wa kawaida ya
kuwa kutanisha watu katika eneo moja ambapo zingetumika dola za kimarekani 1,168,000
jambo ambalo limewapa shauku viongozi wa kanisa hilo duniani kufanya mkutano mwingine kwa njia
ya mtandao.
Mkutano huo ulioendeshwa kwa lugha ya
Kiingereza, Kifaransa, Kireno na kihispaniola ulihusisha video za masaa 48,masaa 12
ya uwasilishaji ambao umesambazwa kwenye vituo vya televisheni vya kanisa hilo.